Jumatatu, 21 Mei 2018

AKAMATWA KWA KUJIITA YEYE NI IGP SIMON SIRRO


Maricha Mniko (30) ambaye ni mtuhumiwa aliyekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Njombe baada ya kufanya utapeli wa kujitambulisha yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiwa mbele ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe, Renata Mzinga alipozungumza  na Waandishi wa Habari mjini Njombe.

JESHI la Polisi Mkoani Njombe linamshikilia mkazi wa Tandala, Wilayani Makete Maricha Mniko (30) ambaye kabila ni Mkurya na kazi yake ni dereva kwa tuhuma za kutaka kufanya utapeli kwa kujiita yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro na anahitaji kupata msaada wa gari ili alitumie kwa ajili ya kwenda nalo mkoani Mara.

Akizungumza kutoka ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Renata Mzinga alisema kuwa mnamo Mei 18, mwaka huu majira ya saa nne asubuhi mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Japanes ya mkoani Njombe, Daniel Hatanaka alipigiwa simu na mwananchi huyo akijitambulisha kuwa yeye ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro.

"Akimweleza kuwa ana matatizo ya kijana wake ambaye anakesi huko Mara, hivyo anahitaji ampatie gari kwa ajili ya kufanya shughuli zake," alisema Renata.

Kamanda huyo alisema baada ya mmiliki huyo kupigiwa simu hiyo, aliweza kumhoji tapeli huyo kujua namba yake ameipata wapi, lakini kwa mujibu wa maelezo ya mtuhumiwa huyo alimweleza kuwa namba ya mmiliki huyo aliipata kupitia kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe.

"Hivyo mmiliki huyo aliamua kuwasiliana na sisi jeshi la polisi na sisi kwa kutupa hiyo namba kwa kuwa tunazitambua hizo namba za mkuu wa jeshi la polisi, tuliona moja kwa moja kuwa siyo namba za mmiliki mkuu wa jeshi la polisi," alisema Renata.

Jumatatu, 22 Januari 2018

WANAWAKE WILAYANI MAKETE WANYIMWA HAKI YA KUMILIKI ARDHI



Na Nyandazajuublog-Makete

IMEELEZWA Wanawake wajane pamoja na wasichana wilayani Makete wamekuwa hawapewi fursa za kuweza kumiliki ardhi wilayano humo, kutokana na kuwepo na mila na desturi kandamizi zinazoendelea baina ya makabila yaliyopo.

Kufuatia hali, Katibu Tawala wa Wilaya ya Makete, Grace Mgeni amewataka wananchi wilayani Makete kuachana na tabia za kuwatenga wanawake ili wasiweze kupata haki za kuwa na ardhi, jambo ambalo alisema linaonyesha dhahiri mwanamke bado anabaguliwa.


Wilayani Makete

Akizungumza mjini hapa, mara baada ya kufungua mkutano wa wadau wa kujadili masuala ya ardhi wilayani Makete ulioandaliwa na Shirika lisilokuwa la kiserikali la MIICO linajishughulisha na utatuzi wa migogoro ya ardhi, Nyanda za Juu Kusini, Grace alikiri kuwa wilayani Makete bado kuna migogoro ya ardhi.

"Katika wilaya yetu ya Makete kuna changamoto ya matumizi bora ya ardhi, hasa katika upandaji wa miti, wananchi wamekuwa wanapanda miti mpaka sehemu ambazo zinatumika kwa ajili ya kilimo cha chakula, mkakati wa wilaya ni kupunguza na kutoa ile miti ambayo imepandwa sehemu zisizostahili," alisema Grace.

"...na pia kwenye umiliki wa ardhi inaonekana mwanamke hajapewa kipaumbele sana kwenye umiliki wa ardhi, jamii itambue mwanamke naye ana haki ya kumiliki ardhi kama mwanaume, tusiwatenge tuwape haki yao," alisema.

Kwa upande wake, Afisa Ardhi wa wilaya ya Makete, Novatus Lyimo alisema kutokana na sheria za kikabila kuendelea kuwepo wilayani Makete, wanawake wamekuwa hawapewi mamlaka ya kumiliki ardhi hivi sasa.

"Sheria nyingi za kimila zinabana haki mwanamke kuweza kumiliki ardhi, tunajaribu kutoa elimu kila tunapopata fursa kuwa mwanamke ana haki ya kumiliki ardhi, lakini kwa Makete bado tunachangamoto ya mwanamke kumiliki ardhi," alisema Lyimo.

"Huku bado kuna sheria za kimila, kikabilia ambazo zinawabana wakina mama, utakutana na swali mtu anakuambia mwanamke akishaolewa, ataenda kupata ardhi kwa bwana yake, lakini akifika pia kule, akifa bwana anarudi kwao, sasa hakuna sehemu ambayo anapata ardhi, hivyo hapa Makete ni changamoto," alisema.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo, hata kwenye mikutano inayoitishwa na maafisa ardhi kwa wananchi kujadili masuala ya migogoro ya ardhi, mwanamke amekuwa akinyimwa haki ya kuongea.
"Saa nyingine mwanamke kuongea kwenye mkutano hawezi kuongea, kwa sababu hizo ndizo zilivyo huku Makete, mwanaume ndiye anapaswa kuongea, kwa hiyo tunapowapa nafasi ya kuongea wanawake huwa wanashangilia sana," alisema Lyimo.

Akizungumzia namna Halmashauri inavyojikita kutatua migogoro ya ardhi wilayani Makete, Lyimo alisema bado migogoro katika halmashauri hiyo ipo licha ya kuendelea kuitatua wakishirikiana na MIICO.

"Kuna migogoro baina ya kijiji na kijiji kutokufahamu mipaka, kwa hiyo katika halmashauri yetu yenye vijiji 93 karibu  vyote vina migogoro, lakini tunaenda awamu kwa awamu, MIICO kwa upande mmoja inatusaidia sana kwa sababu kwa upande wa halmashauri kinachotubana ni bajeti," alisema Lyimo.

Naye Mratibu wa MIICO, Catherine Mulaga alisema katika utatuzi wa migogoro ya wafugaji na wakulima wamefanikiwa kusaidia kupunguza migogoro iliyokuwepo katika kata za Mbalatse na Mfumbi kwa kiasi kikubwa, lakini changamoto kubwa waliyoibaini ipo kwa upande wa wanawake kumiliki ardhi.

"Tulifanya utafiti nakuona kwamba, kulikuwa na changamoto nyingi kwenye masuala ya ardhi ambayo yana athiri, ustawi wa maisha ya mkulima wilaya ya Makete, tulikuta kuna suala la uelewa mdogo wa sheria zinazoongoza masuala ya ardhi," alisema Grace.

"Changamoto nyingine ilikuwa ni kwa upande wa umiliki wa ardhi kwa mwanamke, suala la jinsia limekuwa likijitokeza ambapo wakinamama wengi wamekuwa wakiathiriwa kwenye upatikanaji wa ardhi," alisema.

Jumatatu, 18 Desemba 2017

MKUTANO WA CCM-NEC TAIFA ULIVYOFANA DODOMA


Wajumbe wakijimwayamwaya ukumbini kushangilia wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, akiingia ukumbini


Mwimbaji wa TOT akiimba wimbo wa kuhamasisha mapokezi ya Mwenyekiti ukumbini


Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Jakaya Kikwete na Mwenyekiti mstaafu wa CCM Ali Hassan Mwinyi wakimsubiri Mwenyekiti Kuingia Ukumbini. Mzee Mwinyi akisoma toleo maalum la gazeti la Uhuru wakati akisubiri.


Viongozi waliotangulia meza kuu wakisimama kumlaki Mwenyekiti wa CCM rais Dk John Magufuli wakati akiingia ukumbini.


Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akisalimia viongozi mbalimbali baada ya kuingia ukumbini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana.


Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli akiwa tayari ukumbini. Wengine kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mstaafu Jakaya Kikwete, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa CCM Rais wa Zanzibar Dk. Shein, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM-bara Philip Mangula na Mwenyekiti Mstaaafu wa CCM Benjamin Mkapa.


Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Maguduli akijadili jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana baada ya kuketi ukumbini.


Waimbaji wa TOT wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya Mkutano kuanza.


Wajumbe wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa Taifa.


Mwenyekiti wa CCM Rais Dk John Magufuli na viongozi wengine meza kuu wakiimba wimbo wa Taifa huku wamesimama. 

Jumatano, 28 Juni 2017

Viongozi wawili wa serikali wauawa Kwa Kupigwa Risasi Kibiti


Viongozi wawili wa serikali za mtaa katika Kijiji cha Mangwi wilayani Kibiti mkoani Pwani wameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Jumatano, Juni 28.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga zimeeleza kuwa waliouawa ni Mtendaji wa Kijiji cha Mangwi, Shamte Makawa na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mangwi, Maiko Nicholaus.

Aidha, kamanda wa polisi amesema kuwa tayari askari wamekwenda eneo hilo kwa ajili ya hatua zaidi.

Hadi sasa watu zaidi ya 37 tayari wameuawa katika mfululizo wa matukio ambayo bado Polisi hawajafahamu ni nani mhusika na lengo haswa la kufanya hivyo.

Mwalimu wa Sekondari Ajinyonga kwa Kunywa Sumu


Mwalimu  Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa  wilayani Nkasi   amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni   mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema   mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga  karibu na kituo kikuu cha    mabasi yanayokwenda  mikoani.

Alisema hadi sasa   hajafahami chanzo cha mwalimu huyo kujiua kwa   sumu ingawa aliacha ujumbe uliosomeka, “Kama nadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wangu lakini asilaumiwe, nisilaumiwe chochote juu ya kifo change”.

Inadaiwa kwamba siku ya tukio mwalimu huyo  alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala na baadaye  alikabidhi funguo na kuondoka kwenda kusikojulikana.

Taarifa zinadai   ilipofika usiku wa manane alirejea katika nyumba hiyo akiwa amelewa akachukua ufunguo kwa mhudumu  na kuingia ndani ya chumba chake   kulala.

Baada ya muda mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya mtu akikoroma kwa sauti ya juu hali iliyzua hofu.

Mhudumu   alilazimika kuomba msaada kwa wapangaji wengine waliokuwamo ndani ya nyumba  hiyo na  kuvunja mlango.

Baada ya kuvunjwa kwa mlango mhudumu huyo akiwa na wapangaji hao, walimkuta mwalimu huyo akiwa anatokwa mapovu hali iliyowalazimu kumkimbiza  hospitalini lakini wakiwa njiani alifariki dunia.

RPC Kyando  alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa utabibu,   Mwalimu  Sanga alikunywa sumu.

Wabunge wanawake watengewa chumba cha kunyonyeshea


Bunge limetenga chumba maalum kwa ajili ya wabunge wenye watoto wachanga kunyonyesha watoto wao wakati vipindi vya bunge vinaendelea.

Uamuzi huo umetangazwa leo (Jumatano) bungeni na Naibu Spika Dk Tulia Ackson mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.

"Ofisi ya Bunge inataarifu kuwa imetenga chumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea kwa wabunge wenye watoto wachanga,"amesema.

Amewasihi wabunge wenye watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao angalau miaka miwili kama inavyoshauriwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mtoto wa miaka mitano abakwa Mwanza


Na Veronica  Martine, Mwanza

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.

“Kitendo cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya zamani,” walisema Wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.


Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.

Rais Wa TFF Na Katibu Wake Watiwa Mbaroni

Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao. 

Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao.

Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria.


Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika.

Wengine ni aliyekuwa katibu mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka (FAT sasa TFF), Michael Wambura na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayubu Nyenzi.

Gazeti la Nipashe lilieleza kubaini kuwa, mkutano mkuu wa wanachama wa TFF uliofanyika Desemba 2011 uliidhinisha Kampuni ya Ukaguzi ya TAC kuwa mkaguzi wa hesabu za shirikisho kwa miaka mitano kuanzia mwaka ulioishia Desemba 31, 2011.

Ripoti ya ukaguzi wa kampuni hiyo inaonesha kuwa, katika kipindi cha kuanzia Agosti 15, 2014 hadi Septemba 30, 2015, TFF ililipa jumla ya Sh. milioni 274.072 kwa Wambura na kampuni za Punchlines (T) Ltd na Artriums Dar Hotel Ltd bila kuwa na nyaraka stahiki.

Pia, ripoti ya ukaguzi maalum wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa timu ya taifa (Taifa Stars) iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inabainisha matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa TFF.

Katika ripoti hiyo inaelezwa kuwa, kuanzia Novemba 13, 2013 hadi Februari 15, 2014, jumla ya dola za Marekani 315,577 (sawa na sh. milioni 688.368) zilichotwa kwenye akaunti ya fedha za udhamini wa TBL kwa Taifa Stars na kutumika kinyume cha makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa shirikisho na kampuni hiyo.

Inaelezwa pia kwenye ripoti hiyo kuwa kuanzia Novemba 11, 2013 hadi Machi 11, 2014, jumla ya dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF.

Miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia kinyume fedha hizo ni Malinzi, Matandika, Ali Ruvu, Nyenzi, Ally Mayay, Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara, Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.

Ripoti ya ukaguzi wa TAC inaonesha Wambura alilipwa jumla ya Sh. milioni 67.5, Punchline (T) Ltd ililipwa Sh. milioni 147.154 na Artriums Dar Hotel Ltd ililipwa Dola za Marekani 28,027 (Sh. milioni 59.417).

Aidha, ripoti hiyo inaonesha malipo ya maelfu hayo ya Dola kwa Artrium yalifanyika siku moja ya Machi 4, 2015 kwa TFF kuandika vocha nne zenye namba 001467, 001468, 001469 na 001470, tatu zikiidhinisha malipo ya Dola 9,000 kila moja wakati moja ikiidhinisha malipo ya Dola 1,027.

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa timu ya ukaguzi ilibaini malipo kwa wadau hao wa soka yalifanyika bila idhini ya Kamati ya Utendaji ya TFF.

Jumamosi, 6 Mei 2017

WANAFUNZI PAMOJA NA WALIMU WAO WAFARIKI ARUSHA


Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha.

Jumatatu, 10 Aprili 2017

KINYESI CHA BINADAMU CHAZALISHWA NJOMBE KUBORESHA MAZAO SHAMBANI


 Sehemu ya choo kinachoonyesha namna ya kuvuna
 kinyesi tayari kwa mbolea shambani

Na Michael Katona, Njombe

WAKATI jamii nzima ikielewa kwamba kinyesi cha binadamu kina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, Shirika la SHIPO lililopo mkoani Njombe lenyewe limekuja na mtazamo mwingine kwa kuzalisha kinyesi cha binadamu kuwa mbolea ya kuotesha mazao shambani.

“Kinyesi kibichi cha binadamu kina athari kubwa kwa mwanadamua, lakini kinyesi kilichokauka vimelea haviwezi kuota, hilo ndiyo sababu tunasema kikisha kauka, kinyesi kinaweza kuwa ni mbolea nzuri,” anasema Venance Lulukila, Afisa Maendeleo ya Jamii.

MJANE GRACE: SINA HISIA ZA MAPENZI KWA MIAKA KUMI SASA, NAISHI NA VVU, WANAUME WANANITONGOZA


 Grace Kambindu alipokuwa akihojiwa na waandishi

Na Michael Katona, Njombe

Mwanamke Grace Kambindu “maarufu mama Rose” ni muathirika anayeishi na virusi vya ukimwi mkoani Njombe kwa miaka kumi hivi sasa toka alipogundulika kuwa na ugonjwa huo, lakini pamoja na kuwa na maambukizi ya VVU amesema bado wanaume wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kufanya naye mapenzi.

“Ni wanaume wengi sana wanaonihitaji nifanye nao mapenzi, lakini huwa nawaeleza hisia za mapenzi kwangu mimi zilishatoweka, nafanya kazi nzito hapa nilipo tofauti na uwezo wangu,” anasema Grace.

Alhamisi, 6 Aprili 2017

Spika wa Bunge Aagiza Polisi kumkamata Mbunge Halima Mdee

Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameliagiza Jeshi la Polisi kumkamata na kumfikisha Bungeni Mbunge wa Kawe (CHADEMA) Halima Mdee kujibu tuhuma za kutoa lugha za matusi kwa Spika wakati wa uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki uliofanyika April 4, 2017.

Pia Mbunge Freeman Mbowe ameagizwa na Spika Ndugai kufika mbele ya Kamati ya Maadili leo akituhumiwa kutukana bunge kufuatia uchaguzi huo  wa EALA. 

Mwingine anayetarajiwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge ya Kinga, Maadili na Madaraka leo ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastory Mnyeti ambaye ameitwa na kamati hiyo  na anatakiwa kufika leo. 

Rais Dkt Magufuli Akutana Na Balozi Wa Israel

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalumu toka kwa Waziri Mkuu wa Israel Mhe. Benjamin Netanyahu uliowasilishwa kwake na Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na  Balozi wa Israel hapa nchini Mhe. Yahel Vilan baada ya kutana naye kwa mazungumzo Ikulu jijini Dar es salaam leo April 6, 2017
PICHA NA IKULU

SIRRO; TUMEMKAMATA ALIYEMUUA MPENZI WAKE


JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.

Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;

“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani” ameeleza huku akisema upelelezi unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

Katika hatua nyingine Sirro amesema wamewakamata raia watatu wa kigeni kutoka Afrika Kusini wakiwa na vipande viwili vya meno ya vinavyokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 45 na wafanyabiashara wa madawa ya kulevya ambao walikamatwa Machi 28 mwaka huu maeneo ya Upanga Dar.

Sirro ameeleza kuwa upelelezi juu ya watuhumiwa hao bado unaendelea ili kubaini kama walikuwa wanamiliki nyara hizo za serikali kihalali na mawasiliano kati ya Idara Maliasili yanaendelea.

Jumatatu, 3 Aprili 2017

WANAWAKE LUDEWA WATAKA HAKI SAWA


Wanachama wa MVIWATA wilayani Ludewa wakiwa katika maadhimisho ya wanawake kata ya Mlangali.


Mratibu wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Remmy Urio akiongea na wanachama wa MVIWATA
Mratibu wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Remmy Urio akiongea na wanachama wa MVIWATA 
Mwezeshaji kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani Ludewa Bw.Godwin Lusawo akiongea na wanachama wa Mviwata.
Wanachama wa MVIWATA wilayani Ludewa wakiwa katika maadhimisho ya wanawake kata ya Mlangali. 
Mwenyekiti wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Zebedayo Mgaya akiongea na wanachama wake
 Mgeni rasmi wa maazimisho hayo ambaye pia ni Diwani wa viti maalumu kata ya Mlangali Mh.Agatha kayombo akiwahutubia wanachama wa MVIWATA
Kikundi cha ngoma ya asili ya Ngwaya kutoka kata ya Milo kijiji cha Mavala kijulikanacho kwa jina la Kaza Buti kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
viongozi mbalimbali wakifuatilia jumbe kutoka ktka kikundi cha ngoma ya asili 
Mwenyekiti wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Zebedayo Mgaya akiongea na wanachama wake
  Mgeni rasmi wa maazimisho hayo ambaye pia ni Diwani wa viti maalumu kata ya Mlangali Mh.Agatha kayombo akiwahutubia wanachama wa MVIWATA
Diwani wa viti maalumu wa kata ya Lugarawa Mh.Frolencia Msemwa akisisitiza jambo kwa wanawake wenzake
Kikundi cha ngoma ya asili ya Ngwaya kutoka kata ya Milo kijiji cha Mavala kijulikanacho kwa jina la Kaza Buti kikitumbuiza katika maadhimisho hayo 



 Kikundi cha ngoma ya asili ya Ngwaya kutoka kata ya Milo kijiji cha Mavala kijulikanacho kwa jina la Kaza Buti kikitumbuiza katika maadhimisho hayo 

Wanawake wilayani Ludewa mkoa wa Njombe wamezitaka asasi mbalimbali za kiraia pamoja na Serikali kusimamia haki sawa kwani bado mfumo dume pamoja na mila na Desturi za makabila ya wilaya hiyo zimeendelea kuwakandamiza kwa kuwanyima fulsa mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali.

Hayo yalisemwa na wanawake hao hivi karibuni ktk kijiji cha Mlangali wilayani hapa ikiwa ni siku ya maadhimisho ya mwanamke Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania(MVIWATA) ambapo walisema mpaka sasa kuna baadhi ya wanaume huwazuia wake zao kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali kwa kuhofia kutawaliwa kiuchumi.

Akiongea katika maadhimisho hayo mmoja wa wanawake hao Bi.Frida Mgayamkazi wa kijiji cha Mavala katika kata ya Milo alisema kuwa richa ya Mviwata kujaribu kuwaunganisha wanawake katika mtandao huo wa wakulima ambao ukiwa na malengo ya kuwainua kiuchumi lakini bado hakuna haki sawa kwani baadhi ya wanaume wamekuwa ni kikwazo katika mafanikio ya mwanamke.

Bi.Frida alisema kuwa wanawake walio wengi wilayani Ludewa hasa vijijini wamekuwa wakizuiliwa na wanaume zao kujiunga katika vikundi vya vikoba na siliki,vikundi ambavyo maeneo mengine vimekuwa vikiwasaidia sana wanawake kiuchumi hivyo asasi za kilaia na Serikali ni vyema kujikita vijijini ili kuwaelimisha wanaume hao ambao wanaendekeza mfumo dume kuacha dhana hiyo ambayo inarudisha maeneleo nyuma.

Alisema awali kabla hajajiunga na MVIWATA  hali ilikuwa mbaya sana kiuchumi kwani alishindwa hata kuwanunulia mahitaji ya shule watoto wake kutokana na baadhi ya wanaume kumdanganya mume wake kuwa akimruhusu mke wake kujiunga huko atamzidi kiuchumi na baadaye atamkimbia hali ambayo si kweli.

“walimdanganya sana mume wangu lakini baada ya kupata elimu kutoka mviwata aliniruhusu kujiunga na vikundi mbalimbali na hivi sasa ananufaika kupitia mimi kwani tunasaidiana kwa kila jambo katika familia yetu tofauti na awali nilikuwa nikimtegemea yeye kwa kila jambo,lakini bado majirani zangu wamekuwa wakisema nimemshika mume wangu kwakuwa kaniruhusu kufanya biashara na kujiunga vikundi vya kuweka na kukopa”,Alisema Bi.Frida.

Naye mratibu wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Remmy Urio alisema kuwa ndani ya wilaya ya Ludewa Mviwata inafanya kazi katika kata nne ambazo ni kata ya ,Milo,Lubonde,Lupanga na Mlangali pia kata ya Lugarawa imeanza kuunda vikundi vya wakulima ingawa bado mradi haujafika huko.

Bw.Urio alisema kuwa Mviwata ilianza kufanya kazi rasmi wilaya ya Ludewa mwaka 2011 lakini mpaka sasa imepata mafanikio makubwa kwa kutoa elimu kwa wakulima na kuwatafutia masoko ya mazao yao pia wanawake walio wengi wamenufaika na mpango huo kwani kupitia vikundi vya wakulima wameweza kuunda vikundi vya kuweka na kukopa na kujikuta wanakuwa na maisha bora kiuchumi tofauti na awali. 

Alisema huu ni mwaka wa mwisho kwa mviwata ndani ya wilaya ya Ludewa kutokana na mkataba wa wafadhiri lakini wakikubali kuongeza mkataba basi mradi huo utakwenda katika kata nyingine pia kwani kila mwaka hufanyika kongamano la wanawake na kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni kuelekea Tanzania ya Uchimi wa viwanda ipi nafasi ya mwanamke hivyo wanawake wanapaswa kujitathimini kwa kauli mbiu hii.

Akifunga kongamano hilo la wanawake kiwilaya lililoandaliwa na MVIWATA Mgeni rasmi ambaye pia ni diwani wa viti maalumu kata ya Mlangali kupitia chama cha mapinduzi Mh.Agatha Kayombo alisema kuwa yeye tayari ni mwanachama wa Mviwata hivyo akina baba wanapaswa kuwaruhusu wake zao kujiunga na mviwata na vikundi vingine vya kiuchumi ili kujiinua kiuchumi.

Mh.Agatha alisema kuwa ifikie wakati wanawake wilayani Ludewa waruhusiwe kumiliki ardhi pamoja na mali kwani bado baadhi ya wanaume huona kuwa mwanamke hana haki ya kumiliki ardhi na mali wala kujiunga katika vikundi vya kiuchumi wakati anayetunza familia kwa muda mwingi ni mwanamke .

Alisema kuwa wakati wa kilimo kama huu baadhi ya wanaume wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika unywaji wa pombe za asili na kuwaacha wanawake wakiwa wazalishaji mashambani lakini wakati wa mauzo mwanaume ndiye wakwanza kutafuta wateja wa mazao na mwisho wa siku huuza mazao yote na kutoweka nyumbani na akimuacha mwanamke akihangaika na watoto aliwataka wanawake kusimama kidete katika kusimamia uchumi wa familia.

TFDA YAWANUA WATALAAMU WAKE MKOANI NJOMBE

 AFISA AFYA MKOA WA NJOMBE MATHIAS GAMBISHI AKICHANGIA HOJA


 HAWA NI WASHIRIKI WA KUTOKA  HALMASHAURI ZA MKOA WA NJOMBE AMBAO NI WATALAAM WA AFYA,MAAFISA BIASHARA, MAAFISA KILIMO, ASKALI WA POLISI NA WADAU WENGINE WA TFDA





 MENEJA TFDA KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI BWANA Rodney   Alananga

 MUWAKILISHI WA MKURUGENZI MKUU WA TFDA DKT SIKUBWABO NGENDABANKA AKIZUNGUMZA NA WASHIRIKI WA SEMINA HIYO



 AKIHITIMISHA SEMINA HIYO YA SIKU MBILI KAIM MGANGA MKUU SAMSON SORO SASI
















NJOMBE

Watalaamu Wa Mamlaka Ya Chakula Na Dawa TFDA  Waliopo Kwenye Halmashauri  Wametakiwa Kujenga Tabia Ya Kutoa Taarifa Kila Mwezi Za Kazi Wanazofanya Za  Utafiti Na Ukaguzi wa Maduka  Katika Halmashauri  Za Mkoa Wa Njombe Ili Kutambua Mambo Muhimu Yanayotakiwa Kufanyiwa Kazi.

Rai Hiyo Imetolewa Na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Wa Njombe Dkt  Samson Soro Sasi Wakati Akifunga Mafunzo Ya Siku Mbili Kwa   Watalaamu  Mbalimbali  Wanaounda Kamati  Ya Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Katika Halmashauri Mkoani Hapa.

Dkt Soro Sasi  Amesema Kuwa Kwa Kipindi Chote Kumekuwa Na Changamoto Ya Baadhi Ya Watalaamu  Mbalimbali Wa TFDA Kutoa Taarifa  Pindi Wanapokuwa Wamefanya Kazi Ya Ukaguzi Kwenye Halmashauri Zao  Licha Ya Kufanya Kazi  Ili Kuwawajibisha Watakaokiuka Utaratibu Huo.

Dkt  Soro Sasi Ametaka Washiriki Wa Mafunzo Hayo Yalioandaliwa Na Mamlaka Ya Chakula Na Dawa TFDA Kwa  Watalaamu Wake Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe  Kutumia  Kikamilifu Kama Walivyokumbushwa Kwenye  Mafunzo Hayo Ili Kutoa  Elimu Kwa  Wafanyabiashara  Na Wananchi Juu Ya Kutumia Vyakula  Vilivyopitwa Muda Wake  Wa Matumizi Ya Binadamu.

Akizungumza Mara Baada Ya Kuhitimishwa Kwa Mafunzo Hayo Meneja Wa Mamlaka Ya Chakula Na Dawa Kanda Ya Nyanda Za Juu Kusini Rodney   Alananga  Amesema Mafunzo Hayo Yatasaidia Watalaamu Hao Kufuatilia Majengo Ambayo Hayajasajiliwa, Na Kutoa Elimu Kwa Wananchi Huku Wananchi Nao Kuonesha Ushirikiano Kwa TFDA Ili Kutoa Huduma Bora Ya Chakula Na Dawa.

Nao Baadhi Ya Washiriki Wa Mafunzo Hayo Wameshukuru  Kwa Elimu Iliyotolewa Kwani Kuna Baadhi Ya Mambo Yanayohusu Uingizwaji Wa Bidhaa Zisizosajiliwa  Ambapo Sasa Watakwenda Kugundua Badhaa Bandia Na Zisizobandia Ili Wananchi Wapate Huduma Ya Chakula Kilicho Salama.

Katika Mafunzo Hayo Yaliotolewa Kwa Siku Mbili Yamewahusisha  Wakaguzi Wa Halmashauri Za Mkoa Wa Njombe Wakiwemo  Jeshi La Polisi,Maafisa Afya, Maafisa Biashara,Kilimo Na Mifugo, Wafamasia,Wanasheria, Wahasibu Na Waganga Wakuu Wa Halmashauri Za Wilaya.