Ulimbwende/Urembo/Mitindo

Vazi la Kim Kardashian, Rihanna lashangaza wengi

SHARE THIS
TAGS
Kim Kardashian na kanyeruhanaBADI MCHOMOLO NA MITANDAO
MAVAZI ya mwanamuziki Rihanna na mwanamitindo, Kim Kardashian yamekuwa kivutio na kituko kwa mashabiki wao walipokuwa katika onyesho la Met Gala, huko nchini Marekani.
Kim alikuwa karibu muda wote na mume wake mwanamuziki, Kanye West, huku Rihanna akiwa wa mwisho kuingia katika onyesho hilo akionekana mpweke aliyefunikwa vema na gauni lake lililoonekana kama limemkumbatia.
Wawili hao walionekana katika onyesho la Met Gala, lililohudhuriwa na wasanii wa fani mbalimbali, lakini hata hivyo hawakujali namna watu walivyokuwa wakiwazungumzia.
“Nimeamua kuacha simu yangu nyumbani kwa kuwa nilijua kwamba mashabiki watakuwa na maswali mengi juu ya vazi langu,’’ alisema Kim na kuongeza:
“Nikiwa na shida ya kutumia simu nitatumia ya mume wangu, ninaamini kama ningekuja na simu yangu muda mwingi ningekuwa natumia kutokana na ujumbe kutoka kwa mashabiki.”

MREMBO NYANDA ZA JUU KUSINI AFUNGUKA, APONDA USHINDI WA SITTI, ADAI ULIPANGWA MAPEMA


Na Michael Katona, Njombe



MSICHANA Maureen Godfrey, ambaye ni mrembo wa Nyanda za Juu Kusini, akitokea Mkoa wa Njombe, amefunguka na kudai kuwa ni vigumu kwa warembo kutoka kanda hiyo kuweza kufika hatua ya fainali kwenye shindano la Mrembo wa Tanzania.



Akizungumza baada ya kushindwa kufanya vyema kwenye mashindano ya kumsaka Miss Tanzania, yaliyofanyika Oktoba 11, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, Maureen alisema wakati akiwa anashiriki shindano la 'Miss Nyanda za Juu' mkoani Iringa, aliambiwa na mmoja wa majaji, ambaye anatoka ndani ya Kamati ya Miss Tanzania, kwamba ni ndoto kwa warembo kutoka mikoa ya kusini kuweza kushinda taji hilo.



“Hakuna warembo wazuri na wenye sifa kutoka kanda hiyo, hivyo si rahisi kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuweza kutoa mrembo atakayeweza kutwaa taji hilo,” alisema Maureen akimnukuu jaji huyo (jina tunalo).



Mrembo huyo alisema kwa jinsi ambavyo ameona mashindano ya mwaka huu yalivyoendeshwa na Sitti Mtemvu kuvishwa taji la Miss Tanzania, haoni sababu kwa warembo wengine watakaotaka kushiriki mashindano hayo kwenye kanda ya Nyanda za Juu Kusini kuungana na warembo wengine katika kambi ya Miss Tanzania mwakani.



“Kwa warembo wengine ambao watataka kuja kushiriki kwenye kanda ya Nyanda za Juu Kusini, siwashauri washiriki mashindano haya. Niliwahi kumuuliza jaji mmoja ni kwa nini Nyanda za Juu Kusini mtu akijitihadi sana, anaishia 15 bora? Alinijibu kwa sababu huko kwenu hamna warembo wazuri, na alidai eti wasichana wazuri wako Mwanza, Dar es Salaam na Arusha,” alisema Maureen.



Maureen, ambaye hakuingia hatua ya 15 bora kwenye mashindano ya mwaka huu, yaliyowashirikisha warembo 30 kutoka nchi nzima, alisema warembo wenzake wanaotoka mikoani wamekuwa hawapewi nafasi kama warembo wengine wanaotoka kwenye mikoa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.



“Nilipotangazwa kuwa mshindi wa urembo wa mkoa wa Njombe na Nyanda za Juu Kusini, wapo baadhi waliniona ni mshamba na nisiyekuwa na sifa za kuuwakilisha mkoa kama mrembo, wengine walidai sisi warembo tunaotokea huku Nyanda za Juu Kusini eti tunatokea porini, hatujui lolote,” alisema Maureen.



Mrembo huyo alida wakati akiwa kwenye kambi ya Miss Tanzania, vipaumbele walikuwa wakipewa zaidi warembo kutoka Kanda ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza.

“Mambo mengi nilikuwa naona, wanapewa vipaumbele warembo wanaotoka Arusha, Mwanza, Shinyanga na Dar es Salaam, tena kwa kila kitu, hasa katika suala la mahojiano kwa kila mshiriki, tuliambiwa tutafanyiwa (interview) mara tatu ili tuonekane kwenye luninga, lakini nilimuuliza muongozaji filamu, inakuwaje mtu mmoja anakuwa ni yeye tu anayerekodiwa huku wengine hatupigwi picha za video?



“Muongozaji wa picha alikuwa anamchukua mtu mmoja pekee yake kwa kuanzia mguuni mpaka kichwani, lakini wengine tulikuwa hatupewi nafasi hiyo. Nilimuuliza mbona wengine hatuchukuliwi kama huyo, akasema wengine siyo lazima kuchukuliwa. 

Kama mnasema picha si lazima, basi mngekuwa mnachukua warembo kumi tu ndiyo wanaotakiwa waonekane, kuliko kufanya ubaguzi wa picha na mahojiano kwa warembo wengine, ili hali wakiwa na matumaini ya kufanyiwa interview, lakini imekuwa ni tofauti,” alilalamika mrembo huyo.



Mwakilishi huyo kutoka mkoani Njombe pia aliyakosoa mashindano hayo kwa waandaji kuwanyima warembo wengine nafasi ya kujitambulisha jukwaani, kama ambavyo miaka mingine imekuwa ikifanyika,badala yake ilitumika njia ya kurekodiwa na kurushwa katika luninga kwa kila mshiriki kuonyeshwa anakotoka na vitu ambavyo anapendelea kufanya katika jamii.



“Tulipokuwa tunatoka Moshi kwenda KIA (uwanja wa ndege wa Kilimanjaro), nilihoji ni kwa vipi hatufanyiwi mahojiano sisi baadhi ya warembo huku wengine tayari wamefanyiwa zaidi ya mara tatu. Lakini picha ambayo nilipigwa mimi ni ile ya kujitambulisha unauwakilisha mkoa gani,” alisema mrembo huyo.



Alipoulizwa kama anakubaliana na uamuzi wa majaji kumtangaza Sitti, alisema hakustahili kabisa kuwa mshindi na tayari kulikuwa na dalili za upendeleo za kumtangaza mshindi huyo.



“Huyu dada hakustahili kuwa mshindi wa taji hili la Miss Tanzania, labda pengine alistahili kuwa mshindi wa kawaida kati ya warembo watano bora, mimi napinga yeye kuwa mshindi, kwa sababu tangu awali dalili za upendelo zilishafanyika na alikuwa amepangwa,” alisema Maureen.



"Jambo la kushangaza ni kwa vipi kila mara, mrembo huyo apite katika kila hatua na hata zaidi muda mwingi kamera zilikuwa zikimuonyesha yeye, hii si sawa, matokeo yalipotoka wapo watu waliangua kilio na wengine walipoteza fahamu kwa mshituko mkubwa, ambao hawakuutarajia,” alisema.



Aliwashauri waandaaji a Miss Tanzania, chini ya Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim Lundenga, kuepuka lawama hivi sasa ni bora mashindano hayo yakawa yanafanyika katika miji mingine kuliko miaka yote kufanyika Dar es Salaam pekee.



“Rai yangu ni kwa waandaaji hawa wadogo kwamba wasikatishwe tamaa na haya yaliyotendeka katika shindano hili, lakini pia haki haikutendeka kwa washiriki wengine waliokwenda kushindana. Kama Nyanda za Juu Kusini imeonekana hawana warembo wazuri, nashauri mashindano ya urembo yatakayofanyika kwenye kanda hiyo, yaishie hapo hapo na si kupelekwa kwenye shindano la Miss Tanzania,” alisema Maureen.



"Ni vyema mshindi atakayeshindanishwa kutoka kwenye kanda, apewe zawadi sawa na zile zinazotolewa kwa Miss Tanzania. Hakuna maana ya sisi warembo tunaotoka mikoani, kushirikishwa kwenye fainali hizo. Tumekuwa tunaonekana sisi ni washamba na hatuna sifa zinazostahili,” alilalamika. 



Tayari ushindi wa Sitti umeshaanza kulalamikiwa na wadau wa mashindano hayo, ambapo inadaiwa kuwa, ameghushi umri wake.

Sitti katika fomu za kujiandikisha kuingia katika mashindano hayo, alijaza ana umri wa miaka 18, 

wakati umri wake halisi unadaiwa kuwa ni miaka 25. Sifa za mshiriki wa Miss Tanzania anatakiwa awe na umri wa miaka 18 hadi 23, awe raia wa Tanzania, awe hajaolewa, awe na ufahamu wa kutosha kujieleza, awe hajazaa na asiwe mwanafunzi wa shule ya msingi au sekondari.



Kwa upande wake, Maria Itala, ambaye ni mama mzazi wa Maureen, ambaye alikwenda kushuhudia fainali hizo jijini Dar es Salaam, akizungumza kwa niaba ya wazazi wenzake, alionya kwamba endapo waandaaji hawatakuwa makini, mashindano hayo yatapoteza sifa zake na jamii kuyachukulia kuwa ya kihuni.



“Kufanya mashindano ya kikanda zaidi bila kwenda Taifa, kutasaidia sana washiriki hususan wazazi wanaowakilishwa na watoto wao kwenye fainali hizo, wasipate hasara kubwa kama ambavyo mimi mzazi wa Maureen nilivyopata,” alisema Itala.



Aliishauri Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, kuangalia uwezekano wa kuyasimamia ili kuepuka utata, ambao umekuwa ukijitokeza mara kwa mara, ikiwemo harufu ya rushwa na upendeleo.



“Mashindano haya ni ya kitaifa, ambapo baadaye mwakilishi anapeperusha bendera ya Tanzania kwenye taji la dunia, ni vyema yakadhaminiwa na serikali yenyewe. Rushwa hivi sasa ni kubwa sana kwenye mashindano haya, ni vyema serikali ikachukua jukumu la kudhamini Miss Tanzania, kama ambavyo wanavyofanya nchi za Nigeria, Ghana na nyinginezo, ndiyo maana wenzetu wanapata wawakilishi wanaofanya vizuri kwenye shindano la dunia,” alisema.



“Endapo serikali itayachukua, kwanza itaingiza pato kubwa na vilevile itakuwa inagharamia kila kitu, lakini si kama hivi sasa, wenzetu wanatushangaa, iweje mpaka kwenye mashindano makubwa kama hayo, mzazi aendelee kutoa gharama kubwa za kuchangia maandalizi ya mshiriki? Hapana, hili siyo sahihi, mtoto anapata manyanyaso na kubaguliwa, kweli mzazi unaweza kuugua,” alisema Itala.



Alidai tangu mtoto wake ashiriki kwenye kambi hiyo ya Miss Tanzania, jambo kubwa ambalo amejifunza ni kuona baadhi ya wazazi wenzake wanashindwa uwezo wa kifedha kwenye maandalizi hayo, na hasa kwa baadhi ya warembo wanaotoka katika mikoa hiyo mipya kwa sababu hawafahamiki na hivyo warembo wanaopewa nafasi kubwa ni wale wanaotoka katika kanda fulani.



“Ni vigumu kwa mrembo anayetoka katika hii mikoa mipya kuweza kushinda. Kwanza hajulikani, mashindano ya sasa yanaonekana kuegemea zaidi kwenye kanda fulani, sikubaliani na waandaaji kujikita zaidi kutangaza vivutio vya kanda ya kaskazini, kwani hata nyanda za juu kusini inapaswa kupewa nafasi ya kutangazwa zaidi, pia zipo fursa,” alisema.



Itala pia alitoa tahadhari kwa waandaaji kuachana na kasumba ya upendeleo inayoanza kuonekana hivi sasa kwa mashabiki kutengeneza vipeperushi vya ushabiki kwa mrembo ambaye wanaona atashinda.



“Mtizamo wangu kwa sasa, mashindano haya yameanza kuingizwa na siasa, watu wanakuja na mabango, wengi tumeona wamekuja na vipeperushi vinavyoonyesha tayari mrembo fulani atakuwa mshindi, na hatimaye akawa mshindi, hiyo tayari ni siasa, hatufanyi mashindano ya urembo yakaingizwa siasa,” alisema.

  • Ahaidi kusaidia mapambano dhidi ya VVU
  • Mama Maureen: Tusizuie ndoto za watoto wetu




Na Michael Katona, Njombe

“Msichana kushiriki mashindano ya urembo, si uhuni, na sidhani kushiriki urembo ni kukiuka maadili, ni mchezo kama ilivyo michezo mingine,” anasema Maureen Godfrey, akiwa amekaa na mama yake, Maria Itala, wakati alipofanya mahojiano maalum hivi karibuni.

Maureen, akiwa Miss Redds Mkoa wa Njombe, alifanikiwa kutwaa taji la Miss Redds Nyanda za Juu Kusini baada ya kuwashinda warembo wengine kutoka mikoa ya Iringa, Mbeya, Ruvuma, na Rukwa.

Ni jambo la kujivunia katika Mkoa mpya wa Njombe kutokana na ukweli kwamba ni mara ya kwanza kufanya shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa. Pia Njombe kama mkoa imeshiriki kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kumtoa mshindi wa kuwakilishi kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika shindano kuu la kumtafuta Miss Redds Tanzania mwaka 2014.

“Tatizo kubwa ni mtazamo uliopo hivi sasa kwa jamii kuwa warembo wanapovaa pale jukwaani nusu uchi, ndivyo wanachukulia kwamba mashindano hayo ni ya kihuni, lakini si hivyo, ila ni mrembo mwenyewe inategemea amelelewa namna gani na wazazi wake,” anaongeza kusema Maureen.

Mbali na kuwahimiza wazazi wa mkoa wa Njombe kuwaruhusu mabinti zao kupenda kushiriki mashindano hayo ya urembo, Maureen anasema akiwa balozi wa mkoa wa Njombe kwenye mashindano ya kumsaka Redss Miss Tanzania mwaka huu, ataendeleza kampeni ya serikali kuhamasisha jamii kupitia kwa warembo wenzake kupiga vita maambuki ya virusi vya Ukimwi (VVU).

“Hili suala la ugonjwa hatari wa Ukimwi, sitakuwa nyuma katika kulipigia kampeni ili warembo wenzangu pia watambue kwamba ni hatari kwa jamii, nitakapokuwa kambini, nitasimama na kutoa ushauri nasaha, elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi,” anasema Maureen.

Akizungumzia changamoto ambazo mkoa wa Njombe imekuwa ikishindwa kutoa warembo kutokana na wazazi wengi kutokuwa na mwamko wa kuwaruhusu mabinti zao wanaotaka kushiriki, mama yake mzazi, Itala aliwaasa wazazi wenzake kuachana na imani potofu kuwa urembo ni uhuni.

“Sioni mantiki ya wazazi wenzangu mkoani Njombe na sehemu nyingine kuwakataza warembo wanaotaka kushiriki mashindano, ni wajibu wao sasa wajue msichana anapoguswa kutaka kushiriki wasimzuie,” anasema Itala.

Mama huyo mzazi wa Maureen alitolea mfano alivyofanya kwa mwanae kwa kuamua kumruhusu kushiriki mashindano hayo na hatimaye kushinda taji la Miss Njombe na kuwakilisha Nyanda za Juu Kusini.

“Mwanangu alikuja na kunieleza mama mimi nataka kujaribu kushiriki Miss Njombe, bila hiyana nilimruhusu ashiriki na nilikwenda kushuhudia mashindano, sikuamini wakati matokeo yanatangazwa kwamba mwanangu ndiye Miss Njombe,” anasema Itala.

“Hata alivyokuwa anafanya mazoezi sikuwa na matarajio yoyote, inashangaza sana na hata tulipokwenda kumpa ‘sapoti’ katika mashindano ya Nyanda za Juu Kusini, nako pia nilijikuta nashangazwa ni bahati gani mwanangu ameipata,” anasema Itala.

Mzazi huyo wa Maureen aliwataka wazazi wasiwe wazito kuwatoa mabinti zao pale wanapohitaji kushiriki mashindano hayo, na kwamba jambo la muhimu ni kuwatia moyo katika mashindano hayo.

“Maureen aliniomba niende kuangalia tukio la Miss Kanda, na akanieleza tukija sisi wazazi na marafiki tutamtia nguvu na kufanya vyema, lakini ni maajabu kweli binti yangu amefanya vyema tena katika shindano hilo,” anasema Itala.


“Kitu cha msingi na rai yangu kwa wazazi wenzangu ni kuona ni jinsi gani ambavyo amempa msingi mtoto wake wa kike kutoka awali, kwani mashindano hayo yanalenga kumpa uelewa endapo atashinda basi yeye ndiyo kioo cha jamii,” aliongeza Itala.

Aidha mama Maureen anasema binti yake tangu ashiriki mashindano hayo anaamini ulikuwa ni ushindani, lakini jambo ambalo anapaswa kuliendeleza kwa binti yake ni kumkanya asipotoke kwenye maadili aliyokuwa ametoka kwa kujitambua, eti hivi sasa yeye ni mrembo maarufu.

“Najaribu kumuasa na kumwangalia mwenendo wake, lakini hii yote ni kumchunga asipotoke, na mweleza wewe ni mtoto wa kike unatakiwa kujiheshimu na kujijali na kujitambua katika jamii, tatizo wazazi wengi hasa sisi Waafrika hatuna tabia ya kumuambia mtoto wa kike wazi ni madhara gani anayoweza kuyapata endapo atajiingiza katika mapenzi akiwa mdogo,” anasema.

Mzazi huyo aliwataka wanawake hususan wazazi wa Njombe kuiga mfano alioufanya yeye, wajitoe kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki katika mashindano hayo kwa kuwa yanafaida kwa msichana.

“Mbali na kupata faida yake binafsi, mtoto wangu ameweza kutambulika, lakini pia mashindano hayo yanaleta sifa ya mkoa alikotoka, mfano ameuletea sifa mkoa mpya wa Njombe, lakini pia ameweza kupiga hatua ya kuwa Miss Nyanda za Juu Kusini,” anasema Itala.

Mrembo Maureen ambaye kabila lake ni Mnyakyusa, akizungumzia historia yake ya masomo, anasema elimu ya msingi alianza kuipata kupitia shule ya Arage iliyopo Jijini Mbeya, ambapo baadaye alijiunga na kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya St. Marys iliyopo pia jijini Mbeya.

Baada ya kuhitimu kidato cha nne, hakuweza kufanya vyema na hivyo wazazi wake walimtaka ajiendeleze kwa kuamua kujiunga na masomo katika Chuo cha Tumaini kilichopo Iringa ambapo alichukua masomo ya Biashara, na hivi sasa ni mwaka wake wa mwisho wa kuhitimu masomo hayo ngazi ya Diploma.

Mrembo Maureen katika mashindano ya Redds Miss Tanzania ataiwakilisha Njombe, wakati mrembo Martha John ambaye ni Miss Iringa 2014 na Naba Magambo Miss Ruvuma 2014, ndiyo watakaowakilisha  Nyanda za Juu Kusini kwenye kinyang’anyiro hicho.

Mtazamo na ushauri: Piga namba 0753-827444

Email:princemichaelkatona@gmail.com





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni