ASKOFU wa Jimbo la Kuu la Songea mkoani Ruvuma,
Damian Dallu akizungumza wakati wa misa maalum ya maadhimisho ya kilele cha kongamano la vijana wakatoliki kitaifa mjini Njombe
Vijana wakatoliki kutoka mkoani Iringa wakiwa katika maandamano
Na Mwandishi Wetu
ASKOFU wa Jimbo la Kuu la Songea mkoani Ruvuma, Damian
Dallu amesema vijana wengi wamekuwa wakikosa ajira na kubaki wakilalamika
kutokana na wazee wengi kuendelea kung’ang’ania madaraka na kugoma kustaafu
jambo ambalo linaendelea kusababisha chuki miongoni mwa vijana hao.
Akizungumza jana katika misa maalum ya kufunga
kongamano la Vijana wakatoliki Tanzania (VIWAMA) lililofanyika mkoani hapa na
kuwakutanisha vijana mbalimbali kutoka majimbo 32 kati ya 34 nchini askofu
Dallu alisema wazee ndio wanatakiwa kutumia busara kwa kuanza kustaafu kwa
hiari badala ya kusubiri kuondolewa kwa nguvu.
“ukitaka kufanya kazi fanya, usingojee kuheshimika
leo, utaheshimika baadaye ukitoka, na hili nalisema kwa wale wanaopenda
madaraka hawataki kutoka, inaumiza kabisa, ukichukua wengine pale watahama
hawatakuwa na wewe uliyepita zamani, watakuona ni mwema,” alisema Dallu.
“…ukiwa paroko au padre unafanya kazi pale mahari
usingoje pale wakuambie baba umefaulu sana, nakuambia ni kazi bure, acha waseme
baadaye wakati haupo, na watakuwa wanalinganisha na aliyepo,” alisema.
Askofu Dulla alitumia muda huo kumzungumzia Hayati
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kusema alielewa baada ya kufariki
dunia kuwa yeye ni nani katika safari yake ya kuwa kiongozi nchini.
“MWalimu Nyerere ameeleweka alichofanya baada ya kufa
kwa hiyo ndugu zangu msiogope kuondoka madarakani, mfurahi yale yote mishale
inapowaingia mkitoka itatoka, yatabaki makovu,” alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni