Jumapili, 14 Juni 2015

KINANA AITAKA SERIKALI KURAHISISHA UTOAJI WA LESENI

 Wananchi wa Ngara mjini wakishangilia jambo katika mkutano 
wa hadhara wa CCM
 KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiwahutubia wakazi wa mji wa Ngara Mjini kwenye mkutano wa hadara,Nape Nnauye alisema kuwa hakuna sababu ya Watanzania kuingia kwenye mpasuko kwa sababu ya mchakato wa katiba mpya na kuashauri ni vema mjadala ukafungwa kwenye nyumba za ibada. Amesema inasikitisha unapoona baadhi ya viongozi wa dini badala ya kuhubiri neno la Mungu na kuwaunganisha Watanzania wanatumia nafasi yao kuwagawa wananchi kwa sabababu ya Katiba mpya.
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Abdulrhaman Kinana akiwahutubia wananchi wa Ngara mjini,Kinana ameitaka Serikali kurahisisha utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara , madereva wa magari na bodaboda badala ya kuacha watu wanasumbuka kutafuta leseni umbali mrefu tena kwa gharama kubwa.

Kinana amesema kuwa  moja ya ombi la wananchi hao ilikuwa ni kuomba kurahisishiwa kupata leseni ili kuondoa usumbufu wanaoupata sasa.Alisema Serikali lazima iweke mazingira mazuri ya kutoa leseni kwa wananchi wakiwamo wafanyabishara na madereva bodaboda huku akieleza hakuna sababu ya kutumia gharama kubwa kwa ajili ya leseni.
 
Sehemu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua rasmi Chanjo ya  watoto kuzuia maambukizi ya magonjwa katika kata ya Nyakisasa kijiji cha Kashinga akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani Ngara mkoani Kagera,lengo la ziara hiyo likiwani ni kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 na kuhimiza uhai wa chama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni