Na Veronica Martine, Mwanza
Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa
kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza
na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.
Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio
wamesikitishwa na kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.
“Kitendo cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza
tumekumbwa na nini hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na
miaka ya zamani,” walisema Wananchi.
Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed
Msangi amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea
kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na
kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.
Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la
polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni