Wanachama wa MVIWATA wilayani Ludewa wakiwa katika maadhimisho ya wanawake kata ya Mlangali.
Mratibu wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Remmy Urio akiongea na wanachama wa MVIWATA
Mratibu wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Remmy Urio akiongea na wanachama wa MVIWATA
Mwezeshaji kutoka idara ya Maendeleo ya Jamii wilayani Ludewa Bw.Godwin Lusawo akiongea na wanachama wa Mviwata.
Wanachama wa MVIWATA wilayani Ludewa wakiwa katika maadhimisho ya wanawake kata ya Mlangali.
Mwenyekiti wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Zebedayo Mgaya akiongea na wanachama wake
Mgeni rasmi wa maazimisho hayo ambaye pia ni Diwani wa viti maalumu kata ya Mlangali Mh.Agatha kayombo akiwahutubia wanachama wa MVIWATA
Kikundi cha ngoma ya asili ya Ngwaya kutoka kata ya Milo kijiji cha Mavala kijulikanacho kwa jina la Kaza Buti kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
viongozi mbalimbali wakifuatilia jumbe kutoka ktka kikundi cha ngoma ya asili
Mwenyekiti wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Zebedayo Mgaya akiongea na wanachama wake
Mgeni rasmi wa maazimisho hayo ambaye pia ni Diwani wa viti maalumu kata ya Mlangali Mh.Agatha kayombo akiwahutubia wanachama wa MVIWATA
Diwani wa viti maalumu wa kata ya Lugarawa Mh.Frolencia Msemwa akisisitiza jambo kwa wanawake wenzake
Kikundi cha ngoma ya asili ya Ngwaya kutoka kata ya Milo kijiji cha Mavala kijulikanacho kwa jina la Kaza Buti kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
Kikundi cha ngoma ya asili ya Ngwaya kutoka kata ya Milo kijiji cha Mavala kijulikanacho kwa jina la Kaza Buti kikitumbuiza katika maadhimisho hayo
Wanawake wilayani Ludewa mkoa wa Njombe wamezitaka asasi mbalimbali za kiraia pamoja na Serikali kusimamia haki sawa kwani bado mfumo dume pamoja na mila na Desturi za makabila ya wilaya hiyo zimeendelea kuwakandamiza kwa kuwanyima fulsa mbalimbali zikiwemo za uzalishaji mali.
Hayo yalisemwa na wanawake hao hivi karibuni ktk kijiji cha Mlangali wilayani hapa ikiwa ni siku ya maadhimisho ya mwanamke Duniani yaliyoandaliwa na Mtandao wa vikundi vya wakulima Tanzania(MVIWATA) ambapo walisema mpaka sasa kuna baadhi ya wanaume huwazuia wake zao kujiunga na vikundi vya uzalishaji mali kwa kuhofia kutawaliwa kiuchumi.
Akiongea katika maadhimisho hayo mmoja wa wanawake hao Bi.Frida Mgayamkazi wa kijiji cha Mavala katika kata ya Milo alisema kuwa richa ya Mviwata kujaribu kuwaunganisha wanawake katika mtandao huo wa wakulima ambao ukiwa na malengo ya kuwainua kiuchumi lakini bado hakuna haki sawa kwani baadhi ya wanaume wamekuwa ni kikwazo katika mafanikio ya mwanamke.
Bi.Frida alisema kuwa wanawake walio wengi wilayani Ludewa hasa vijijini wamekuwa wakizuiliwa na wanaume zao kujiunga katika vikundi vya vikoba na siliki,vikundi ambavyo maeneo mengine vimekuwa vikiwasaidia sana wanawake kiuchumi hivyo asasi za kilaia na Serikali ni vyema kujikita vijijini ili kuwaelimisha wanaume hao ambao wanaendekeza mfumo dume kuacha dhana hiyo ambayo inarudisha maeneleo nyuma.
Alisema awali kabla hajajiunga na MVIWATA hali ilikuwa mbaya sana kiuchumi kwani alishindwa hata kuwanunulia mahitaji ya shule watoto wake kutokana na baadhi ya wanaume kumdanganya mume wake kuwa akimruhusu mke wake kujiunga huko atamzidi kiuchumi na baadaye atamkimbia hali ambayo si kweli.
“walimdanganya sana mume wangu lakini baada ya kupata elimu kutoka mviwata aliniruhusu kujiunga na vikundi mbalimbali na hivi sasa ananufaika kupitia mimi kwani tunasaidiana kwa kila jambo katika familia yetu tofauti na awali nilikuwa nikimtegemea yeye kwa kila jambo,lakini bado majirani zangu wamekuwa wakisema nimemshika mume wangu kwakuwa kaniruhusu kufanya biashara na kujiunga vikundi vya kuweka na kukopa”,Alisema Bi.Frida.
Naye mratibu wa MVIWATA wilaya ya Ludewa Bw.Remmy Urio alisema kuwa ndani ya wilaya ya Ludewa Mviwata inafanya kazi katika kata nne ambazo ni kata ya ,Milo,Lubonde,Lupanga na Mlangali pia kata ya Lugarawa imeanza kuunda vikundi vya wakulima ingawa bado mradi haujafika huko.
Bw.Urio alisema kuwa Mviwata ilianza kufanya kazi rasmi wilaya ya Ludewa mwaka 2011 lakini mpaka sasa imepata mafanikio makubwa kwa kutoa elimu kwa wakulima na kuwatafutia masoko ya mazao yao pia wanawake walio wengi wamenufaika na mpango huo kwani kupitia vikundi vya wakulima wameweza kuunda vikundi vya kuweka na kukopa na kujikuta wanakuwa na maisha bora kiuchumi tofauti na awali.
Alisema huu ni mwaka wa mwisho kwa mviwata ndani ya wilaya ya Ludewa kutokana na mkataba wa wafadhiri lakini wakikubali kuongeza mkataba basi mradi huo utakwenda katika kata nyingine pia kwani kila mwaka hufanyika kongamano la wanawake na kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni kuelekea Tanzania ya Uchimi wa viwanda ipi nafasi ya mwanamke hivyo wanawake wanapaswa kujitathimini kwa kauli mbiu hii.
Akifunga kongamano hilo la wanawake kiwilaya lililoandaliwa na MVIWATA Mgeni rasmi ambaye pia ni diwani wa viti maalumu kata ya Mlangali kupitia chama cha mapinduzi Mh.Agatha Kayombo alisema kuwa yeye tayari ni mwanachama wa Mviwata hivyo akina baba wanapaswa kuwaruhusu wake zao kujiunga na mviwata na vikundi vingine vya kiuchumi ili kujiinua kiuchumi.
Mh.Agatha alisema kuwa ifikie wakati wanawake wilayani Ludewa waruhusiwe kumiliki ardhi pamoja na mali kwani bado baadhi ya wanaume huona kuwa mwanamke hana haki ya kumiliki ardhi na mali wala kujiunga katika vikundi vya kiuchumi wakati anayetunza familia kwa muda mwingi ni mwanamke .
Alisema kuwa wakati wa kilimo kama huu baadhi ya wanaume wamekuwa wakitumia muda wao mwingi katika unywaji wa pombe za asili na kuwaacha wanawake wakiwa wazalishaji mashambani lakini wakati wa mauzo mwanaume ndiye wakwanza kutafuta wateja wa mazao na mwisho wa siku huuza mazao yote na kutoweka nyumbani na akimuacha mwanamke akihangaika na watoto aliwataka wanawake kusimama kidete katika kusimamia uchumi wa familia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni