Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha.
Mkasa huo umetokea takribani kilomita 25 kutoka katika geti la hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ,takriban kilomita 150 kutoka mji wa Arusha.
Orodha ya majina ya wanafunzi waliofariki katika ajali hiyo
Wanafunzi hao walikuwa wamesalia na kilomita 5 ili kufika sehemu
waliokuwa wakielekea.
Taarifa za awali kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo
mwalimu ilisema kuwa basi hilo lilikuwa limebeba wanafunzi na waalimu
wanaosadikiwa kuwa thelathini na tano.
Mwandishi wa BBC mjini Arusha Ally Shemdoe, aliyeko mkoani humo
amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mvua kali inayoendelea kunyesha katika
eneo hilo.
Anasema kwamba dereva alidaiwa kutoijua barabara hiyo hivyobasi
alikosa mweleko na kuteleza kando ya barabara kabla ya kutumbukia korongoni
katika mto Malera.
Wanafunzi na waalimu hao walikuwa safarini kuelekea Karatu
kwenye shule ya Tumaini English Medium Junior Schools kufanya mtihani wa kanda
wa majaribio ya kujipima uwezo kabla ya kufanya mtihani wa taifa wa darasa la
saba wa Kanda.
Shule hizo mbili zimekuwa zikifanya utaratibu wao wa kawaida,
Taarifa kutoka katika hospitali ya Lutheran Karatu, kwa muujibu
wa Mbunge Ester Mahawe aliyeko hospitalini hapo , ni kuwa maiti zilizopokelewa
katika hospitali hiyo ni 32 hii ikiwa na maana , miongoni mwao waalimu wawili,
dereva mmoja , na wanafunzi ishirini na tisa.
Kati ya wanafunzi waliopoteza maisha yao 10 ni wa kiume huku 18
wakiwa wasichana.
Aidha maiti zitahifadhiwa katika hospitali ya Mkoa wa Arusha,
Mount Meru.
Mkuu wa wilaya ya Arusha , Fabian Dagalo amewataka wananchi kuwa
watulivu kutokana na tukio hilo baya, na kwamba serikali itatoa taarifa baadaye
kuhusiana na msiba huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni