Jumatano, 28 Juni 2017

Mwalimu wa Sekondari Ajinyonga kwa Kunywa Sumu


Mwalimu  Betson Sanga aliyekuwa akifundisha Shule ya Sekondari Milundikwa  wilayani Nkasi   amefariki dunia baada ya kunywa sumu akiwa katika nyumba ya kulala wageni   mjini hapa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando alisema   mwalimu huyo alifariki dunia juzi usiku huku akiwa ndani ya chumba alichokuwa amepanga  karibu na kituo kikuu cha    mabasi yanayokwenda  mikoani.

Alisema hadi sasa   hajafahami chanzo cha mwalimu huyo kujiua kwa   sumu ingawa aliacha ujumbe uliosomeka, “Kama nadaiwa deni lolote na mtu amweleze mkurugenzi ambaye ni mwajiri wangu lakini asilaumiwe, nisilaumiwe chochote juu ya kifo change”.

Inadaiwa kwamba siku ya tukio mwalimu huyo  alifika katika nyumba hiyo ya kulala wageni na kupanga chumba kwa ajili ya kulala na baadaye  alikabidhi funguo na kuondoka kwenda kusikojulikana.

Taarifa zinadai   ilipofika usiku wa manane alirejea katika nyumba hiyo akiwa amelewa akachukua ufunguo kwa mhudumu  na kuingia ndani ya chumba chake   kulala.

Baada ya muda mhudumu wa nyumba hiyo alisikia sauti ya mtu akikoroma kwa sauti ya juu hali iliyzua hofu.

Mhudumu   alilazimika kuomba msaada kwa wapangaji wengine waliokuwamo ndani ya nyumba  hiyo na  kuvunja mlango.

Baada ya kuvunjwa kwa mlango mhudumu huyo akiwa na wapangaji hao, walimkuta mwalimu huyo akiwa anatokwa mapovu hali iliyowalazimu kumkimbiza  hospitalini lakini wakiwa njiani alifariki dunia.

RPC Kyando  alisema kwa mujibu wa uchunguzi wa utabibu,   Mwalimu  Sanga alikunywa sumu.

Wabunge wanawake watengewa chumba cha kunyonyeshea


Bunge limetenga chumba maalum kwa ajili ya wabunge wenye watoto wachanga kunyonyesha watoto wao wakati vipindi vya bunge vinaendelea.

Uamuzi huo umetangazwa leo (Jumatano) bungeni na Naibu Spika Dk Tulia Ackson mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni.

"Ofisi ya Bunge inataarifu kuwa imetenga chumba maalum kwa ajili ya kunyonyeshea kwa wabunge wenye watoto wachanga,"amesema.

Amewasihi wabunge wenye watoto wachanga kuwanyonyesha watoto wao angalau miaka miwili kama inavyoshauriwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mtoto wa miaka mitano abakwa Mwanza


Na Veronica  Martine, Mwanza

Mtoto mmoja mwenye umri wa miaka mitano anasadikiwa kubakwa katika eneo la Kabuholo kata ya Kirumba wilayani Ilemela ijini Mwanza na kijana mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kisha kutokomea kusikojulikana.

Wakizungumzia tukio hilo baadhi ya wananchi katika eneo la tukio wamesikitishwa na kitendo hicho cha kikatili dhidi ya mtoto huyo.

“Kitendo cha kikatili jamani kwani sisi wakazi wa Mwanza tumekumbwa na nini hatuelewi kwani vitendo vya kinyama vimeshamiri tofuati na miaka ya zamani,” walisema Wananchi.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa kutokana na kijana huyo kufanya unyama huo kisha kutokomea kusikojulikana amesema jeshi la polisi linaendelea kumtafuta mtuhumiwa huyo na kwamba atakapokamatwa sheria itafuata mkondo wake.


Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuhakikisha mtuhumiwa huyo anatiwa nguvuni.

Rais Wa TFF Na Katibu Wake Watiwa Mbaroni

Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao. 

Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao.

Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria.


Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika.

Wengine ni aliyekuwa katibu mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka (FAT sasa TFF), Michael Wambura na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayubu Nyenzi.

Gazeti la Nipashe lilieleza kubaini kuwa, mkutano mkuu wa wanachama wa TFF uliofanyika Desemba 2011 uliidhinisha Kampuni ya Ukaguzi ya TAC kuwa mkaguzi wa hesabu za shirikisho kwa miaka mitano kuanzia mwaka ulioishia Desemba 31, 2011.

Ripoti ya ukaguzi wa kampuni hiyo inaonesha kuwa, katika kipindi cha kuanzia Agosti 15, 2014 hadi Septemba 30, 2015, TFF ililipa jumla ya Sh. milioni 274.072 kwa Wambura na kampuni za Punchlines (T) Ltd na Artriums Dar Hotel Ltd bila kuwa na nyaraka stahiki.

Pia, ripoti ya ukaguzi maalum wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa timu ya taifa (Taifa Stars) iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inabainisha matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa TFF.

Katika ripoti hiyo inaelezwa kuwa, kuanzia Novemba 13, 2013 hadi Februari 15, 2014, jumla ya dola za Marekani 315,577 (sawa na sh. milioni 688.368) zilichotwa kwenye akaunti ya fedha za udhamini wa TBL kwa Taifa Stars na kutumika kinyume cha makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa shirikisho na kampuni hiyo.

Inaelezwa pia kwenye ripoti hiyo kuwa kuanzia Novemba 11, 2013 hadi Machi 11, 2014, jumla ya dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF.

Miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia kinyume fedha hizo ni Malinzi, Matandika, Ali Ruvu, Nyenzi, Ally Mayay, Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara, Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.

Ripoti ya ukaguzi wa TAC inaonesha Wambura alilipwa jumla ya Sh. milioni 67.5, Punchline (T) Ltd ililipwa Sh. milioni 147.154 na Artriums Dar Hotel Ltd ililipwa Dola za Marekani 28,027 (Sh. milioni 59.417).

Aidha, ripoti hiyo inaonesha malipo ya maelfu hayo ya Dola kwa Artrium yalifanyika siku moja ya Machi 4, 2015 kwa TFF kuandika vocha nne zenye namba 001467, 001468, 001469 na 001470, tatu zikiidhinisha malipo ya Dola 9,000 kila moja wakati moja ikiidhinisha malipo ya Dola 1,027.

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa timu ya ukaguzi ilibaini malipo kwa wadau hao wa soka yalifanyika bila idhini ya Kamati ya Utendaji ya TFF.

Jumamosi, 6 Mei 2017

WANAFUNZI PAMOJA NA WALIMU WAO WAFARIKI ARUSHA


Ajali mbaya ya gari imetokea kaskazini mwa Tanzania , ambapo basi aina ya Costa mali ya shule ya Lucky Vincent iliyoko eneo la kwa Mrombo ,limetumbukia katika mto Marera ulioko katika mlima Rhotia, , Karatu mkoani Arusha.

Jumatatu, 10 Aprili 2017

KINYESI CHA BINADAMU CHAZALISHWA NJOMBE KUBORESHA MAZAO SHAMBANI


 Sehemu ya choo kinachoonyesha namna ya kuvuna
 kinyesi tayari kwa mbolea shambani

Na Michael Katona, Njombe

WAKATI jamii nzima ikielewa kwamba kinyesi cha binadamu kina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, Shirika la SHIPO lililopo mkoani Njombe lenyewe limekuja na mtazamo mwingine kwa kuzalisha kinyesi cha binadamu kuwa mbolea ya kuotesha mazao shambani.

“Kinyesi kibichi cha binadamu kina athari kubwa kwa mwanadamua, lakini kinyesi kilichokauka vimelea haviwezi kuota, hilo ndiyo sababu tunasema kikisha kauka, kinyesi kinaweza kuwa ni mbolea nzuri,” anasema Venance Lulukila, Afisa Maendeleo ya Jamii.

MJANE GRACE: SINA HISIA ZA MAPENZI KWA MIAKA KUMI SASA, NAISHI NA VVU, WANAUME WANANITONGOZA


 Grace Kambindu alipokuwa akihojiwa na waandishi

Na Michael Katona, Njombe

Mwanamke Grace Kambindu “maarufu mama Rose” ni muathirika anayeishi na virusi vya ukimwi mkoani Njombe kwa miaka kumi hivi sasa toka alipogundulika kuwa na ugonjwa huo, lakini pamoja na kuwa na maambukizi ya VVU amesema bado wanaume wamekuwa wakimtongoza kwa nia ya kufanya naye mapenzi.

“Ni wanaume wengi sana wanaonihitaji nifanye nao mapenzi, lakini huwa nawaeleza hisia za mapenzi kwangu mimi zilishatoweka, nafanya kazi nzito hapa nilipo tofauti na uwezo wangu,” anasema Grace.