Jumanne, 20 Desemba 2016

UNICEF NA EQUIP WASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MASHULENI.


Mwakilishi wa UNICEF Dkt Jamal Gulaid (kushoto) akimkabidhi majarida ya mazingira Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Stephen Bushiri wakati wa semina elekzi kuhusiana na utunzaji wa mazingira kwenye mkoa wake. 
Miongoni mwa wajumbe wa semina . 

Na Ripota wa Globu ya Jamii, Morogoro.

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulika na watoto UNICEF pamoja Taasisi iliyo chini ya shirika la World Vision yaani Education Quality Improvement Program ( Equip) kwa pamoja wameweza kuendesha semina elekezi kwa wadau wa mazingira mahala pa kazi wakiwemo maafisa maendeleo ya jamii,maafisa ustawi wa jamii, walimu , mabwana afya, pamoja na watendaji kutoka wilaya ya morogoro katika uboreshaji wa mazingira ya kufanyia kazi pamoja na mazingira ya wananchi kwa ujumla. 

Semina hiyo ni pamoja na kutambua umuhimu wa mazingira ktk maisha ya binadamu ambapo Mkurugenzi wa UNICEF Salvatory Mwakibibi na Mjumbe toka Equip, Erasto Henjewele kwa nyakati tofauti wameweza kutoa semina hiyo elekezi ambayo imewataka wajumbe wa semina kuwajibika kikamilifu katika uboreshaji wa mazingira na utunzaji wa mazingira kwa kushiriki upandaji wa miti kipindi hiki cha mvua ktk maeneo yao ya kazi yaliyopendependekezwa kwaajili ya shughuli hiyo . 

Pia suala la utunzaji wa vyanzo vya maji kwa kuelimisha wananchi kutofanya shughuli zozote za kibinadamu ambavyo huharibu mazingira na kusababisha ukame. 

Semina hiyo imekuja baada ya kuonekana mkoa wa morogoro umekumbwa na ongezeko la watumiaji wakubwa wa mkaa na kuni hivyo Taasisi mbalimbali zimefikia hatua ya kuamua kuendesha mafunzo na kushiriki kwenye upandaji wa miti mahala pa kazi ili kupunguza jangwa ambalo linawezakujitokeza siku za mbele. 

Mafunzo hayo yanaambatana pamoja na uteuzi wa mwakilishi kuteuliwa kutoka kila kata ambaye ataenda kupata mafunzo zaidi ya uhifadhi misitu kutoka kwa wataalamu wa maliasili wa Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma,hifadhi inayopakana na ziwa Tanganyika na kwa kipindi chote cha semina wajumbe wameombwa kuwa makini kushiriki zoezi hadi mwisho ili kwenda kuleta ufanisi wa kiutendaji watakaopoenda kusimamia zoezi la upandaji wa miti mahala pa kazi na maeneo maalumu yaliyotengwa kwaajili upandaji huo. 

Ifahamike Equip wamekua wakitoa mafunzo zaidi katika masuala ya kielimu lakini kwa sasa wamefika mbali zaidi hadi kushirikiana na UNICEF kwa kutambua umuhimu wa uboreshaji wa mazingira ya kujifunzia hivyo mwanafunzi au mtoto anayepata elimu kuanzia shuleni hadi maisha ya nyumbani ana uwezo mkubwa wa kuondoka tatizo la uharibifu wa mazingira.

Uongozi wa Taasisi ya Equip katika picha pamoja na wajumbe wa UNICEF wa pili kutoka kulia ni mwakilishi Dkt Jamal Gulaid akifuatiwa na katibu Tawala Mkoa wa Morogoro moro,Stephen Bushiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni