Jumanne, 20 Desemba 2016

MWIGULU NCHEMBA AINGILIA KATI SAKATA LA MAUAJI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI MKOANI PWANI


 Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba kushoto akiwa na Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka wakizungumza jambo baada ya kulikagua gari ambalo lilikamatwa likiwa na wahamiaji haramu 150  Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ambao ni raia wa Ethiopia.
Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mwigulu Nchemba wa kulia na kushoto kwake ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha  mjini Silvestry Koka  wakiangalia gari ambayo ilikamatwa Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani ikiwa na wahamiaji haramu wapatao  150 ambao ni  raia  kutoka nchini Ethiopia ambao walikamatwa wakati wakiwa  wapo safari kuelekea mikoa ya kusini. (PICHA NA VICTOR MASANGU).


NA VICTOR MASANGU, PWANI

KUTOKANA na kuwepo kwa ongezeko la wimbi la migogoro ya ardhi kila kukicha katika baadhi ya maeneo katika Mkoa wa Pwani kati ya jamii ya wakulima na wafugaji na kupelekea wakati mwingine kuibuka kwa mapigano ya wenyewe kwa wenyewe ambayo yanasababisha hali ya uvunjifu wa amani na baadhi ya viongozi na wananchi wengine kupoteza maisha kikatili kimeundwa kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kuweza kukomesha kabisa vitendo hivyo.

Matukio ya namna hiyo katika Mkoa wa Pwani yanaonekana kumsikitisha na kumlazimu Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba kuingilia kati sakata hilo kwa kutangaza rasmi kupambana vilivyo na watu wote ambao watabainika wanajihusisha na vitendo hivyo vya mauaji ili waweze kukamatwa haraka na kuweza kufikishwa katika vyombo vya dola ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Waziri nchemba ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea askari polisi, magereza, uhamiaji pamoja zimamoto wa Mkoani Pwani kwa ajili ya kuweza kukagua shuguli mbali mbali za utekelezaji ya majukumu yao ya kila siku ikiwemo na kuweza kubaini changamoto zinazowakabili pamoja na kuweka mikakati kwa ajili ya kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

“Kumekuwepo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kuna baadhi ya viongozi wa vijiji pamoja na wakulima na wafugaji kupoteza maisha, kwa hili sisi kama Wizara hatuwezi kulivumilia hata kidogo kwani kwa sasa tumejipanga ii kuweza kuwabaini watu ambao wanahusika katika vitendo hivyo,”alisema Waziri.

Alisema kuwa anasikitishwa kuona mauaji yanafanyika kitu ambacho ni kinyume kabisa na sheria na taratibu za nchi, kwa mwananchi yoyote kuamua kujichukulia sheria mikononi kwa kufanya vitendo vya mauaji hivyo ameahidi kulivalia njuga suala hilo na wale wote watakaobainika wataweza kuchukuiwa hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni