Jumanne, 20 Desemba 2016

BAADA YA UZINDUZI, SASA NI SHOO KATIKA KUMBI MBALIMBALI- FELLA


Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Taarab, Mwanahawa Ally akitumbuiza kwenye usiku wa uzinduzi wa bendi ya Yah TMK Taarab.
Mwanamuziki wa Taarabu, Omar Tego akitumbuiza kwenye usiku wa uzinduzi wa bendi ya Yah TMK Taarab. 
wanamuzi wa bendi ya Yah TMK Taarab wakitoa burudani.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

UONGOZI wa bendi ya mpya ya muziki wa taarab nchini 'Yah TMK Modern Taarab', umewataka wapenzi wa muziki huo, kuipokea bendi yao ambayo inaanza rasmi maonyesho yake ya katika kumbi mbalimbali hapa nchini. 

Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella,alisema kuwa mara baada ya kufanya utambulisho wa bendi yao uliyofanyika Jumamosi kwenye Ukumbi wa Dar Live, Yah TMK inaanza rasmi maonyesho yake katika kumbi mbalimbali za burudani hapa nchini. 

Fella alisema bendi hiyo itaanza onesho lake la kwanza Desemba 23 mwaka huu kwenye ukumbi wa CCM Kigamboni wakati mkesho wa Christmas watakuwa kwenye Ukumbi wa Mpo Africa uliopo Tandika. 

Alisema Desemba 25 bendi hiyo itakuwa ndani ya ukumbi wa Lekem uliopo Buguruni na siku ya Desemba 26 itakuwa na Lanch Time Mazense. Fella alisema kuwa bendi yao imejipanga kutoa buriuudani ya aina yake kama wapenzi waliyokuja kwenye utambulisho walivyojionea. 

"Lengo ni kutoa burudani nasi tumejipanga kutoa burudani ya aina yake, wanamuziki wapo vizuri na kila mtu anajisikia kufanya kazi yake kivizuri kabisa"alisema Fella. 

Bendi hiyo yenye wanamuziki mbalimbali nguli, akiwepo Mwanahawa Ali, Fatma Mcharuko, Aisha Vuvuzela, Omar Tego, Mauwa Tego na wapiga vyombo Mohamed Mauji, Mussa Mipango, Chid Boy (kinanda) na Babu Ally Kichupa. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni