Jumamosi, 17 Desemba 2016

MAKAMU WA RAIS ATOA MIEZI MITATU KWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUVIRUDISHA VIWANJA VYOTE VYA WAZI VILIVYOUWA


Makamu wa Rais, Mh. Samia Hassan Suluhu (katikati), Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa tatu kushoto), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dkt. Hamis Kigwangala (kulia) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakiwa katika kampeni ya kufanya mazoezi katika viwanj vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.


Habari kwa hisani ya mwandishi Chalila Kibuda ,
 Globu ya  Jamii.

MAKAMU wa Rais, Samia  Hassan Suluhu amewaagiza Wakuu wa Mikoa nchini pamoja na Wakuu  kutangaza siku ya Jumamosi ya pili ya mwanzo wa mwezi kuwa siku maalum ya  kufanya mazoezi ya kukimbia kwa lengo la kuondokana na magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo yanatokana na mtu kutofanya mazoezi.

Hata hivyo,  Makamu wa Rais, amewaagiza pia viongozi hao wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha ndani ya miezi mitatu  wanavirudisha viwanja vyote vya michezo walivyoviuza ili viweze kuwasaidia wananchi katika kufanyia mazoezi au kutafuta maeneo mengine ya wananchi kufanyia mazoezi.

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo  leo, Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa  kampeni ya kufanya mazoezi nchini ili kujikinga na magonjwa yasiyo ya kuambikizwa katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Amesema kwa sasa serikali imebaini kuwa magonjwa mengi yasiyo ya  kuamuikizwa yamechangiwa na watu kutofanya mazoezi hivyo ameagiza  viongozi hao kuhakikisha wanatenga siku hiyo hali ambayo inaweza kupunguza magonjwa hayo.

"Nawataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kila Jumamosi ya pili ya mwenzi iwe siku ya kufanya mazoezi katika wilaya na vitongoji kwa kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwenye maeneo yao kufanya mazoezi ya mbalimbali  ili iweze kuwasadia’’amesema Makamu wa Rais Samia Hassan  Suluhu.

Amesema anafahamu kuna tatizo kwenye Halmashauri mbalimbali kuwa  wameuza   viwanja vya wazi na kuwaagiza  watendaji wa Halmashauri  ndani ya miezi mitatu kuvirudisha viwanja hivyo kwa ajili ya mazoezi hata kama wakishindwa wametakiwa kutangaza maeneo mengie ili wananchi wayatumie kufanya  mazoezi.

Kwa upande wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Dk. Ali Hassan Mwinyi, amewataka watanzania kupenda kufanya mazoezi kwani njia hiyo itawasaidia katika kuongeza siku za kuishi na kufanikiwa kujikinga na magonjwa mbali  mbali. "Nawaambia siri ya umri wangu  ufanyaji mazoezi kwani mimi kila siku natenga dakiki 90 za kufanya mazoezi kila nikiamka’amesema Rais Mstaafu". Mzee Mwinyi.

Nae Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kwa sasa hali inatisha kwani magonjwa mengi yasiyo ya kuambukizwa yameongezeka na yanasababishwa na kutofanya mazoezi jambo analodai limewasukuma kuandaa kampeni hiyo ya kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ili waweze kujikinga na magonjwa.

Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, pamoja na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia  Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga wakati wa kampeni ya kufanya mazoezi leo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyanyakazi wa mfuko huo katika uzinduzi wa kampeni ya kufanya mazoezi leo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni