Jumamosi, 17 Desemba 2016

BONDIA FRANCIS CHEKA APIGWA KWA TKO RAUNDI YA 3 JIJINI NEW DELHI, INDIA

Bondia Vijender Singh leo amefanikiwa kulinda ubingwa wake wa WBO Asia Pacific Super-Middleweight kwa kumtoa Francis Cheka wa Tanzania kwa TKO raundi ya tatu katika uwanja wa Thyagaraj Stadium jijini New Delhi, India. 
Vijender, aliyenyakua medali ya shaba katika michezo ya Olympiki mwaka 2008 huko Beijing, China, hajawahi kupoteza mchezo katika michezo minane aliyocheza.
Kwa mujibu wa tipota wa Globu ya Jamii huko New Delhi, mpambano huo uliovutia mamia ya mashabiki, refarii ilibidi asimamishe mpambano katika raundi ya 3 baada ya Cheka kuzidiwa.
Francis Cheka na mpinzani wake Vijender Singh wa India wakijinadi kabla ya pambano lao
Bondia Vijender Singh akishangilia ushindi wake dhidi ya Francis Cheka katika   pambano lao la raundi 10 la WBO Asia Pacific Super-Middleweight

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni