Urais 2015: Wassira atinga makao Makuu CCM kuchukua fomu ya Urais
Mpekuzi blog
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira leo amekabidhiwa fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi huku kipaumbele chake kikubwa kikiwa ni kuinua kilimo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari hivi sasa katika ukumbi wa mikutano wa makao makuu Wassira amesema ikiwa atachaguliwa kuwa rais ataboresha kilimo kwa kutumia zana za kisasa huku akisisitiza kuwa jembe la mkono litawekwa katika vyumba ya makumbusho ili iwe historia.
Kwa upande wa ufisdi amesema ufisadi ni wizi,anausikia tu na kwa sababu atakuwa rais atahakikisha kuwa anawachukulia sheria pamoja na kuziongea nguvu sheria ili kupambana nao.
Akizungumzia Muungano amesema atatetea na kuulinda maana kuuvunja ni kugawa nchi.
Mpekuzi blog
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni