Jumatano, 3 Juni 2015

Mazungumzo ya awali kabla ya mkutano wa wanausalama mitandao uliokamilika jijini Johannesburg nchini afrika kusini yanaweza kusomeka kwa"KUBOFYA HAPA"  Mkutano ambao uliokua na vuta nikuvute kupata suluhu ya changamoto tulizo nazo za kiusalama mtandao duniani kote zinazoendelea kukua kila kukicha huku ikionekana dhahiri kabisa wahalifu mtandao wanaelekea kuzidi nguvu huku Tanzania ikiorodheshwa kua ya sita kwa nchi zinazotegemewa kuathirika zaidi na uhalifu mtandao barani Afrika.

Akitolea ufafanuzi wa takwimu hizi Bwana Vernon Frye, Mkuu wa Usalama mitandao wa kampuni ya Vodacom ya Afrika kusini, alielezea kuhusiana na uhalifu mpya wa Ransomware ambapo tayari athari zake zimesha onekana Nchini huku aki ibua mjadala mzito wa wapi tume jikwaa.


Aidha Mjadala mrefu kutoka kwa aliyekua Mkurgenzi wa wakala wa usalama wa Marekani (National Security Agency – NSA) bwana William Binney pamoja na Raisi na muanzilishi wa kivinjari cha aina ya Tor kinachotumika sana na jumuia ya wana usalama mitandao waliibua changamoto ya ufaragha baina ya watumiaji wa mitandao na namna ya kuendelea kuhakiki kunapatikana uthibiti wa faragha hizi kutotumika vibaya na wahalifu.

Nikiwasilisha mada ya changamoto tulizo zazo barani Afika na nini kifanyike ili kujikwamua katika hali mbaya tuliyo nayo hivi sasa ya wimbi la uhalifu mtandao barani afrika ambapo umeendelea kugharimu bara katika Nyanja za kisiasa, kijamii pamoja na kiuchumi. Nilielezea kwa kina mambo ya msingi tunayo takiwa kuyafanyia kazi ili kuhakiki Bara linabaki salama.

Katika mjadala huu ambapo wanausalama mtandao kutoka maeneo mbali mbali ya dunia waliunga mkono nilicho zungumza kua bado kuna kusua sua katika ushirikiano wa pamoja katika kutokomeza uhalifu mtandao huwa wahalifu mtandao kuonekana niwenye ushirikiano ulimkubwa kabisa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni