Alhamisi, 4 Juni 2015

Nkurunziza aahirisha Uchaguzi

 wa Rais na Wabunge

Mpekuzi blog

Serikali ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge uliotarajiwa kufanyika Ijumaa hii umehairishwa mpaka tarehe nyingine itakapopangwa.
 
Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe amesema  kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.
 
Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu baada ya kuwa rais kwa miaka 10.
 
Umoja wa Mataifa imeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongeza idadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi na kukimbilia nchini Tanzania.
 
Hata hivyo umoja wa Afrika mashariki unadaiwa kushindwa  kutoa amri dhidi ya Rais Nurunziza kutokana na kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani kinyume  na katiba ya nchi hiyo suala linalopingwa vikali na wananchi wa nchi hiyo.
Mpekuzi blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni