Alhamisi, 28 Mei 2015

ZITTO AWAONYA VIONGOZI ACT-WAZALENDO

Zitto awaonya viongozi ACT-Wazalendo

SHARE THIS
TAGS
Zitto Kabwe-ACT Leader3Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameionya sekretarieti ya uongozi wa chama hicho na kuitaka kuishi kwa maadili kwa kuzingatia katiba ya chama na kuitekeleza kwa vitendo.
Amesema uadilifu umekuwa ni changamoto kubwa katika nchi hali inayowafanya watanzania washindwe kuaminiana katika masuala mbalimbali.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam juzi alipofungua mkutano wa kwanza wa sekretarieti ya uongozi wa chama hicho.
Alisema iwapo watashindwa kuishi katika maadili mazuri yenye kufuata katiba na sheria za nchi watakiweka chama katika wakati mgumu.
Hatari kubwa kwa chama hicho ni wanachama wake kubeba mazoea ya maisha waliyokuwa wakiishi katika vyama vyao vya zamani na kuyaleta ndani ya ACT-Wazalendo, alisema.
Zitto alisema litakuwa ni jambo la ajabu kwa kiongozi wa chama hicho kuficha taarifa zake za mali na hali hiyo ikaanikwa na watu walio nje ya chama
“Tumevuka vihunzi vingi kuanzia kutafuta usajili wa muda na hata wa kudumu, kuzindua chama na sasa kuwa na sekretariti ya chama. Hatua zote hizo zilikuwa na changamoto nyingi ninyi mmekuwa wateule wa kwanza itunzeni historia hiyo,”alisema Zitto na kuongeza:
“Ni kawaida watu wa karibu kufanya makosa na kulindana lakini makosa hayo hayo yakifanywa na watu wengine waliowalinda wenzao wanakuwa wa kwanza kupiga kelele. Jambo hili halitakubalika ndani ya ACT-Wazalendo na ni lazima tuwe tofauti na hali hiyo”.
Zitto alisema wanachama wa ACT-Wazalendo wanapaswa kutambua kuwa msingi wa kuwapo chama hicho ni kukosekana demokrasia katika vyama vingine na wajiandae kisaikolojia kupata upinzani utakaoendana na kashfa kutoka kwa wasiopenda ushindani wa demokrasia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni