Alhamisi, 28 Mei 2015

KAMATI YA USHAURI MKOA WA MBEYA YAPITISHA MAPENDEKEZO YA KUGAWA MAJIMBO

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akizungumza katika kikao cha kamati ya ushauri cha Mkoa wa Mbeya,(RCC)kimetupilia mbali mgawanyo wa majimbo manne ya uchaguzi ambayo yalipendekezwa kugawanywa kwa ajili ya uchaguzi  mkuu kwa mwaka 2015 baada ya kukosa sifa na vigezo vilivyopendekezwa na Tume ya uchaguzi kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa (Picha na Fahari News)








KAMATI ya ushauri ya Mkoa wa Mbeya (RCC) imepitia na kupitisha mapendekezo ya Halmashauri za Mkoa huo ya kugawa majimbo na mengine kubadili majimbo ya uchaguzi.

Akifafanua katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola jijini Mbeya, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro alisema kikao hicho kimekubaliana na baadhi ya mapendekezo na mengine kuyakataa.

Kandoro alisema mapendekezo hayo yamezingatia vigezo vilivyotolewa ambavyo ni idadi ya watu katika jimbo na hali ya Kijografia ambayo inamuwia vigumu  Mbunge mmoja kuwafikia wananchi wake kwakati ikiwa ni pamoja na mawasiliano.

Aliyataja majimbo waliyokubaliana kuyagawa kuwa ni pamoja na Jimbo la Mbozi Magharibi linalogawanywa kupata majimbo ya Momba na Tunduma, Mbozi Mashariki inkuwa na majimbo ya Vwawa na Mbozi.

Kandoro alisema jimbo lingine lililopitishwa kugawanywa ni Jimbo la Mbeya vijijini linalokuwa na Jimbo la Santilya na Mbeya vijijini na kufafanua kuwa Jimbo hilo linakosa kigezo cha idadi ya watu lakini kutokana na hali ya Jografia na mawasiliano ni vigumu kuongozwa na Mbunge mmoja.

Aliongeza kuwa Majimbo mengine yamebadilishwa majina kutokanana mapendekezo ya Halmashauri ambayo ni Jimbo la Rungwe Mashariki kuwa Jimbo la Busokelo na Jimbo la Rungwe Magharibi kuwa jimbo la Rungwe.

Alisema Majimbo mengine yaliyopendekezwa na halmashari ni pamoja na Halmshauri ya Jiji la Mbeya lakini wazo lao limekataliwa kutokana na kukosa vigezo ambavyo ni kuwa na idadi ndogo ya watu, kuwa na mawasiliano mazuri na ukubwa wa eneo linalofikia kilomita za mraba 214.

Aliongeza kuwa vigezo vingine vinavyoifanya Halmashauri ya jiji kushindwa kugawanywa ni kutokana na kutokuwa na changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, muingiliano wa mamlaka kwa majimbo mawili kuwa chini ya Halmashauri moja.

Alisema Jimbo la Kyela pia limekosa kigezo cha kugawanywa hivyo litaendelea kubaki jimbo moja kama ilivyokuwa awali likiungana na majimbo ya Ileje, Lupa,Songwe na Mbarali.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni