Mhe. Membe akiendelea na mkutano wake na Waandishi wa Habari
Viongozi wan chi za AFRIKA Mashariki wanatarajia kukutana ili kujadili mgogoro wa kisiasa unaoendelea nchini BURUNDI.
Maandamano ya kupinga hatua ya rais PIERRE NKURUNZINZA kugombea urais kwa awamu ya tatu yamekuwa yakiendelea mjini BUJUMBURA.
Waandamanaji wameahidi kuendelea na maandamano yao hadi hapo NKURUNZINZA, atakapotangaza rasmi kuwa hana mpango wa kugombea urais.
Maandamano ya kupinga rais NKURUNZINZA kugombea tena urais, mara kadhaa yamekuwa yakiambatana na ghasia, pamoja na vifo. Mamia ya wananchi wa BURUNDI, wamelazimika kukimbilia nchi jirani, wakihofia usalama wao.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni