VURUGU ZA RAIA NA POLISI NJOMBE
MAITI WAMEACHA KIJIJINI WACHACHE WAMERUDI NJOMBE KUFUATILIA UKWELI WA KIBALI KWA MKUU WA WILAYA YA NJOMBE
Hatimaye Mwili Wa Marehemu Basili Mwalongo Ambaye Amedaiwa Kuuwawa Na Watu Wanaosadikika Kuwa Ni Polisi Katika Mtaa Wa Kambalage Mjini Njombe Umeshindwa Kuzikwa Hadi Muda Huu Kufuatia Wananchi Wa Kijiji Cha Lugenge Kugomea Kuuzika Kutokana Na Kibali Cha Mazishi Kuwa Hakina Mhuri Wa Serikali Wala Sababu Ya Kifo Chake.
Wakizungumza Na Uplands Fm Wananchi Na Ndugu Wa Marehemu Basili Mwalongo Wamesema Kuwa Mwili Wa Marehemu Ulipokelewa Mei 20 Majira Ya Usiku Ukiwa Umepelekwa Na Watu Wasiyofahamika Kuwa Ni Akina Nani Na Kwenye Gari La Mtu Binafsi Na Kuwapatia Kibali Cha Mazishi Ambacho Hakina Taarifa Sahihi Za Kifo Cha Marehemu.
Wamesema Kuwa Baadhi Ya Wananchi Na Wanandugu Wa Marehemu Wakiwa Wameongozana Na Viongozi Wao Wamelazimika Kurudi Katika Ofisi Ya Mkuu Wa Wilaya Ili Waweze Kupatiwa Ufumbuzi Wa Tatizo Lao Na Kufahamu Sababu Iliyofanya Kibali Kutolewa Pasipo Sababu Ya Kifo Cha Marehemu Pamoja Na Kibali Hicho Kuwa Hakina Mhuri Wowote Wa Serikali Kuidhinisha Kutambua Kutokea Kwa Tukio Hilo.
Kwa Upande Wake Kamanda Wa Jeshi La Polisi Mkoa Wa Njombe Franco Kibona Alipofuatwa Na Waandishi Wa Habari Ili Kutolea Ufafanuzi Juu Ya Tukio Lililotokea Mei 19 Na Mei 20 Alisema Hayuko Tayari Kulizungumzia Tukio Hilo Kwa Siku Ya Leo Hadi Kesho Mchana Ikiwa Ni Siku Ya Pili Kamanda Huyo Anafuatwa Na Waandishi Wa Habari Lakini Anashindwa Kutolea Ufafanuzi Wa Tukio Hilo.
Tukio Hilo La Mauaji Limetokea Mei 19 Majira Ya Saa Tatu Usiku Baada Ya Kijana Mmoja Kuuwawa Kwa Risasi Na Mwingine Kujeruhiwa Na Risasi Na Watu Wanaosadikika Kuwa Ni Askali Wa Polisi Ambao Wanadaiwa Kwenda Na Gari La Polisi Katika Kilabu Cha Nyondo Kilichopo Mtaa Wa Kampalage Wakiwa Wamevaa Mavazi Ya Kiraia Na Kutekeleza Mauaji Hayo Jambo Ambalo Lilisababisha Wananchi Kwenda Kibena Na Kufunga Barabara Na Kulazimika Kutumia Mabomu Ya Machozi Kutawanya Wananchi Hao.
JANA HALI ILIKUWA HIVII HAPA CHINI TAZAMA KWANZA
Askari wa FFU Njombe wakifungua barabara kuu ya Njombe - Iringa iliyofungwa kwa kuchomwa mataili na waandamanaji hao
Mmoja Kati ya majeruhi wa vurugu za FFU na Raia leo MANDELE MKAZI WA RAMADHANI AMBAYE NI MWENDESHA PIKIPIKI MAARUFU KAMA BODABODA BAADA YA KUKAMATWA NA FFU KWENYE VURUGU HIZO
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni