Alhamisi, 14 Mei 2015

Mwanaume Afumaniwa Gesti Na Mke Wa Rafiki Yake

Mwanaume Afumaniwa Gesti Na Mke Wa Rafiki Yake

Mpekuzi blog

Kashikashi za kuambiwa umefumaniwa zisikie kwa mwenzako tu! Utakuta mtu mkubwa, bonge, lakini akidaiwa amefumaniwa, nguvu zote zinakwisha! Sijui kwa nini?!

Mfanyabiashara mmoja wa jijini Arusha ‘pedeshee’ aliyejulikana kwa jina la Aldina Hashim, mkazi wa Unga Limted, amechezea kichapo baada ya rafiki yake kipenzi, Emmanuel Mwambije kudai amemfumania na mke wake, Felista Mwambije.

Kwa mujibu wa Mwambije mwenyewe, tukio hilo la aibu lilijiri kwenye gesti moja iliyopo eneo la Makao Mapya jijini hapa ambayo jina linahifadhiwa kwa sasa huku mfumaniaji huyo na timu yake wakishughulika na mfanyabiashara huyo waliyedai ni mgoni wao.

Madai hayo yanasema kuwa, mfanyabiashara huyo alishushiwa kipigo cha haja baada ya kukutwa ndani ya gesti hiyo, tena akiwa mtupu  na mke wa rafiki yake huyo anayefanya kazi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ‘NSSF’ jijini hapa.

Akizungumzia tukio hilo huku akiwa na uso wenye maumivu ya hisia, Mwambije alisema kuwa, Hashimu alikuwa rafiki yake mkubwa (urafiki umekufa) ambapo wakati yeye anafunga ndoa na Felista, alishiriki kumsaidia katika shughuli za hapa na pale.
  
Akishushiwa kichapo.

Mwanaume huyo aliendelea kudai kuwa, baada ya ndoa, maisha na mkewe yaliendelea lakini hivi karibu, alishangaa kupata habari kutoka kwa watu aliokataa kuwataja majina kwamba, rafiki yake huyo anatoka na shemeji yake.
 
“Nilishangaa sana, lakini pia nilishtuka. Kwani Hashim ni rafiki yangu kipenzi. Taarifa nilizozipata ni kwamba, amekuwa akimtongoza mke wangu tangu mwaka jana (2014) kwa kumtumia meseji (SMS) za mapenzi.”

Mwambije alisema baada ya kusikia taarifa hizo, alimbana mkewe, akakiri. Akajiongeza adhabu gani ampe rafiki yake huyo, akaona hakuna nyingine zaidi ya kumwandalia fumanizi la kukata na shoka kwa kuandaa mtego kupitia jamaa zake na kulishirikisha jeshi la polisi.

Kwa kauli ya Mwambije, ina maanisha kwamba kulikuwa na ushirikiano mkubwa  kati yake na mkewe, Felista ili kufanikisha fumanizi hilo.

Mwambije alisema siku ya tukio, Mei, 10, mwaka huu, majira ya saa 7 mchana yeye na ‘skwadi’ yake walivamia kwenye gesti hiyo na kuwanasa wawili hao wakiwa watupu huku Felista akifanikiwa kuchoropoka na kutokomea kusikojulikana.
 
Akisimulia mazingira ya tukio la unasaji, mwanaume huyo alisema, awali rafiki yake huyo aliwasiliana na mke wake majira ya mchana na kukubaliana kukutana eneo hilo na kwamba baada ya kufika na kuingia chumbani mkewe, alimkuta jamaa akimsubiri kwa shangwe kama siyo nderemo.

Mwambije alisema mkewe baada ya kufika ndani ya chumba cha gesti, aliagiza chipsi kuku kwanza na kuomba akaoge kabla ya kuingia kwenye sita kwa sita akiwa ndani ya kanga moja tu ili kuvuta muda wa mumewe kufika!!
 
Muda mchache wakiwa watupu, mume na timu yake, sanjari na polisi walivamia chumba hicho na kumtoa nje mtuhumiwa huyo na kuanza kumwangushia kipigo cha hasira za; ‘kwa nini unaniibia mke wangu?’ Licha ya urefu na uimara wa mwili, mtuhumiwa huyo hakuonekana kufanya makeke zaidi ya kuelemewa.
 
Hata hivyo, wakati wa kipigo hicho, polisi walifanya kazi ya ziada kuzuia hasa baada ya kumsikia, mwana timu mmoja akisema maneno ya kuashiria kutaka kumfanyia kitu mbaya mtuhumiwa huyo.

Akizungumza na na  gazeti la Amani kwa njia ya simu kuhusiana na tukio hilo, Felista alikiri kukutwa chumba cha gesti na rafiki huyo wa mumewe na kusema kuwa, alilazimika kumweleza mumewe kuhusu jamaa huyo kutokana na usumbufu aliokuwa akiupata kutoka kwa rafiki yake.
  
...Akiingizwa kwenye gari la polisi.
Alisema: “Huyo bwana amekuwa akinitongoza kwa muda mrefu sana. Tena amekuwa akiniambia niombe talaka yeye atanioa kwa vile mume wangu hana pesa za kunitunza.
 
“Jumamosi alinipigia simu, nikamwambia mumewe wangu, nikatoka kwetu Ilboru kwa kupanda usafiri wa Toyo na kumfuata mahali aliponielekeza. Nilimkuta ameshavua nguo na kubaki na shuka la gesti, ndipo mume wangu na wenzake walipovamia,” alisema mwanamke huyo.
  
Hata hivyo, katika Kituo Kikuu cha Polisi, mtuhumiwa huyo aliachiwa kwa dhamana huku akipangiwa tarehe ya kurudi tena kituoni hapo.

Chanzo: Gazeti  la  Amani/Gpl

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni