Sentensi nane za Mbunge Edward Lowassa wakati anatangaza kugombea Urais leo May 30 2015 Arusha
May 30 2015 inakuwa siku ambayo inaingia kwenye Historia kubwa kwenye ishu za siasa Tanzania.. Bado miezi michache ufanyike Uchaguzi Mkuu, mmoja ya watu ambao walitajwa sana na kuwa kwenye headlines kubwa kwenye vyombo vya habari ni Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid katikati ya Jiji la Arusha umeshuhudia kwa mara nyingine kujaa kwa watu ambao walikuja kwa ajili ya kushuhudia Mbunge huyo akitangaza nia rasmi kabisa kwamba atagombea Urais mwaka huu.
“Watanzania wanahitaji mabadiliko, nina uwezo wa kusimamia mabadiliko hayo.. Mwalimu Nyerere alisema Watanzania wasipoyapata mabadiliko hayo ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Sina shaka tukijipanga vizuri ndani ya CCM tunaweza kuwapa Watanzania mabadiliko wanayoyataka”>>> Edward Lowassa.
“Nchi yetu inahitaji viongozi wenye sifa hizi.. uongozi wenye uthubutu usioogopa kufanya maamuzi magumu, uongozi usioyumba.. Aweze kuwaunganisha Watanzania na kutoa utofauti kati ya walio nacho na wasio nacho“>>> Edward Lowassa.
“Nina hamu, nina shauku na nina uwezo wa kuiongoza Tanzania… Ninaamini nina kila kigezo cha kuibeba dhamana ya nchi yetu.. Katika vitu ninavyojivunia ni pale nilipoenda kupigana vita ya Kagera, nilishiriki kikamilifu nikiwa miongoni mwa askari wa mbele kuikomboa nchi yetu, muwaulize wengine waliwahi hata kufika Kagera?”>>> Edward Lowassa.
Sauti yake iko hapa, ukiplay utasikia hotuba yake yote
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni