Jumamosi, 30 Mei 2015

TIZAMA DK SLAA ALIVYOANZA ZIARA YAKE, AKABIDHIWA UCHIFU

Kiongozi wa Machifu wa Kabila la Wanyiha, Greenwell Msangawale akimvisha vazi maalum la kichifu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa na kupewa jina 'Mwene wa Mbozi' ambapo pia alikabidhiwa silaha ya jadi aina ya mundu wakimtuma kazi ya kuendeleza vita dhidi ya ufisadi na ubadhirifu nchini ambao umekuwa moja ya sababu za umaskini wa Watanzania. Tukio hilo limefanyika kwenye Uwanja wa Ichenjezya, Vwawa, wilayani Mbozi, Mkoa wa Mbeya ambapo kiongozi huyo amefanya mkutano wa hadhara baada ya kukagua zoezi la uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR. 


 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni