Mkurugenzi wa Shirika la Daraja Development Ltd, Simon Mkina akizungumza na kuwakaribisha waandishi wa habari kutoka Kigoma Press Club (KGPC) walipotembelea ofisi za shirika hilo ambalo ni wachapishaji wa gazeti la Daraja Letu lenye makao yake mjini Njombe.
Mwenyekiti wa Kigoma Press Club, Deogratius Nsokolo akizungumza wakati walipotembelea ofisi za Shirika la Daraja Development Ltd kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.
Na Mwandishi Wetu, Njombe
Timu ya Waandishi wa Habari kutoka Chama Cha Waandishi wa
Habari mkoani Kigoma (KGPC) imefanya ziara siku tatu katika Shirika la Daraja
Development Ltd ambao ni wachapishaji wa Gazeti la Daraja Letu lenye makao yake
makuu mkoani Njombe, huku lengo kuu likiwa ni kubadilishana uzoefu wa kazi
katika nyanja ya habari na masoko.
Katika ziara hiyo, viongozi wa KGPC walioko katika mafunzo
hayo ni Mwenyekiti wa KGPC, Deogratius Nsokolo, Jacob Ezekiel Ruvilo ambaye ni
Mhariri wa Gazeti la Kigoma Yetu, Fadhil Abdallah (Afisa Masoko wa gazeti la
Kigoma Yetu na Katibu Mkuu Msaidizi wa KGPC), Emmanuel Matinde (Mhariri wa
Michezo gazeti la Kigoma Yetu) na Mwajabu Hoza (Mweka Hazina Kigoma Yetu).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni