Zoezi la kuwatambua maiti waliofariki katika ajali ya basi la Majinja iliyotokea katika eneo la changarawe wilayani mufindi hapo jana linaendelea katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa na hospitali ya wilaya ya mufindi ambapo ndugu wa marehemu wameendelea kumiminika kuwatambua ndugu zao.
Taarifa iliyotolewa asubuhi ya leo na Mganga mkuu wa mkoa wa iringa Dokta Robert Salim imeeleza kuwa jumla ya maiti 26 wa ajali hiyo wamehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa iringa na maiti wengine walihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya wilaya ya mufindi,Ambapo mmoja wa majeruhi Oswald Mwinuka amefariki Dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.Mpaka muda huu waliofariki dunia wamefikia 43.
Tupia R.IP yako kama ishara ya kuwaaga hawa ndugu zetu waliotangulia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni