Jumatatu, 23 Machi 2015

TAPELI IKULU AKAMATWA, ATAPELI VIGOGO WENGI

Ikulu 

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata tapeli maaufu hapa jijini anayeitwa Haroub Mtopa miaka 44 mkazi wa mbagala rangi tatu ambaye amekuwa akiwatapeli watu mbalimbali kwa kutumia jina la Katibu wa Rais Jakaya Kikwete, Prosper Mbena kuwatapeli wananchi mbalimbali. Anaandika KAROLI VINSENT,Endelea nayo.

Akithibitisha kumkamata tapeli huyo leo Jijini Dar es Salaam Wakati wa mkutano na waandishi wa Habari,Kamishna wa kanda maalum ya polisi Mkoa wa Dar es Salaam,kamishna Suleiman Kova amesema mtu huyo alikamatwa na maofisa wa usalama walioko Ikulu ambapo walimnasa kutokana na yeye kuwa na tabia ya kwenda ikulu hapo mara mara kwa bila ya kutokuwa na kazi yeyote.

Kamishna Kova ameongeza kuwa tapeli huyo amekuwa na tabia kwenda na wananchi  mpaka nje ya mlango wa kuingia wa ikulu na kuwaacha nje huku akijifanya anaingia ndani ikulu ili kuwaaminisha wananchi hao kwamba anafanya kazi ikulu.

 KamishIna Kova.
Aidha,kamishna Kova amesema mtu huyo amekuwa akizitapeli ofisi mbali mbali za Kiserikali kwa kutumia njia hiyo ya kutumia jina la Mbene pamoja na wananchi.

Vilevile Kamishna Kova amesema siku ya kumkamata walimwekea mtego ndipo ikawa rahisi wao kumkamata.ambapo kamishna kova akawataka wananchi kuwa makini na watu wa aina hiyo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni