Jumatatu, 23 Machi 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, ITV NA MENGI WAPEWA UJUMBE MZITO

Reginard Mengi: Mwenyekiti Mtendaji wa IPP

Na Abel Sichembe  

ITV USIVAE KOTI LA TBC LINA CHAWA, ENDELEA KUWA SUPER BLAND NO.1 TZ:
Kituo cha television cha ITV kwa muda mrefu sasa kimejizolea sifa ya kuwa kituo cha TV kinachoangaliwa zaidi nchini Tanzania. ITV imekuwa ikitoa habari bila kupendelea upande wowote tofauti na ilivyo kwa vituo vingine mfano TBC1.
Lengo la bandiko hili si kukosoa mwenendo wa chombo hicho kinachomilikiwa na kampuni ya IPP media, bali ni kutahadharisha ili kisifuate njia ambayo vyombo vingi hufuata hasa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu na kupoteza mvuto mbele ya watazamaji wake. Nitaweka sababu chache zinazonifanya nianze kuamiani kuna mazingira yanayoelekea kuwa kikwazo kwa ITV kundelea kuwa chombo huru.

1. SERIKALI KUVIBANA VYOMBO YA HABARI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU KUTOA HABARI ZA UPINZANI.
Ni kawaida kwenye nchi za Africa serikali kuviamuru vyombo vya habari (hasa kuelekea kwenye chaguzi) ili visitoe habari za wapinzani wao na kulazimishwa kutoa habari za vyama tawala tu. [mfano ni nchi ya Congo DRC]. Kuna wakati hutunga sheria kandamizi dhidi ya vyombo vya habari kwa manufa ya watawala. Pia hutumia hata mabavu kuvifungia vyombo ambavyo viko huru na ambavyo hukosoa mwenendo mbaya wa watawala kama walivyofanya kwa gazeti pendwa la MwanaHalisi.

2. USHIRIKIANO WA MENGI NA VIONGOZI WA SERIKALI NA CCM.
Siku za hivi karibuni kumekuwa na ushirikano usio wa kawaida kati ya mmliliki wa makampuni ya IPP ndugu Reginald Mengi na vigogo kadhaa wa serikali na Chama Cha Mapinduzi CCM.
Ki msingi sio kosa kwa mtu yeyote kushirikiana na viongozi wa Serikali au chama chochote cha siasa, lakini kuna matukio yasiyo ya kawaida kwa siku za hivi karibuni yanayotia shaka. (1) Kitendo cha ndugu Mengi kuwa karibu na Lowassa mpaka kufikia kutoa msaada wa mamilioni kwenye shule moja amabayo ilipata janga jimboni Monduli {kwa Edward Lowassa} kinafanya baadhi ya wachambuzi wa mambo kuhusisha msaada huo na mbio za kulekea Ikulu ambapo baadhi yao wanasema, mafisadi wanaweza kuitumia fursa hiyo kuhakikisha wanaikamata ITV na IPP kwa ujumla. (2) Kukutana na Waziri mpya wa Nishati na madini mh. George Simbachawene wakati wa kukabidhiana ofisi na waziri aliyepita mh. Sospeter Mhongo (ambaye wakati wa uongozi wake alikuwa haelewani na ndugu Mengi) hasa kutokan na kiu yake ya kutaka kuwekeza kwenye gesi [ambacho ni kilio cha wawekezaji wengi wa kitanzani] hii pia inatia wasiwasi kuwa wataka urais kupitia CCM wanaweza kutumia mwanya wa kumuahadi kuwekeza baada ya wao kuingia madarakani kwa masharti ya kuibana ITV. (3) Kuwepo kwa tetesi kwa kuwa ndugu Mengi ni miongoni mwa watu wanoifadhili (au wanaotarajiwa) kuifadhili CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa October 2015. Hayo ni baadhi ya mambo yanayonifanya nitoe tahadhali mapema kwa ITV, IPP na ndugu Reginald Mengi.

3. UWEZEKANO WA BUNGE KUTUNGA SHERIA KALI YA HABARI.
Kuna habari kuwa inawezekana mswada wa kuvibana vyombo vya habari kwa kisingizio cha vyombo vinavyotoa habari za uchochezi ukawasilishwa bungeni na waziri wa Habari michezo na utamaduni kabla ya kuvunjwa kwa bunge ili kudhibiti vyombo vilivyo huru kama ITV na magezeti yanayo anika madudu ya Serikali na chama tawala.

WAPINZANI JIANDAENI.
Wito wangu kwa CHADEMA/UKAWA ni kujinda kuelekea uchaguzi mkuu ili kuhakikisha wananchi wanapata habari sahihi na kamili kuanzia kampeni, zoezi la kupiga na kuhesabu kura mpaka kutangazwa kwa matokeo ya mwisho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni