Mwanamke mmoja muuzaji dawa za kulevya
anakabiliwa na adhabu ya kifungo baada ya kukutwa akiwa amesheheni dawa za
kulevya aina ya Cocaine katika sidiria yake yenye kipimo cha ukubwa wa 46d.
Nola Williams,mwenye umri wa miaka
47,alisimamishwa katika uwanja wa ndege wa Gatwick ,akitokea Jamaica akiwa na
mtoto mdogo pamoja na muuza unga mwenziwe aitwaye Raymond Goodison mwishoni mwa
mwezi january mwaka huu.
Williams and Goodison alikamtwa na polisi
alipokuwa akitaka kupanda ndege kutoka uwanja wa ndege wa Gatwick kuelekea
Victoria mji ulioko kati kati mwa London.
Tukio hili limeng’amuliwa na polisi walipokuwa
wakifanya ukaguzi kwa wasafiri na hivyo kugundua kilo moja ya kokeini ikiwa
imeshonewa kwenye sidiria ya Nola .
Goodison, alikuwa akikabiliwa na makosa kama
hayo ya usafirishaji mihadarati aliachiliwa baada ya kulipa fidia na kuikimbia
Uingereza hapo awali.
Nola Williams anasubiri kifungo chake ,wakati
Goodison alihukumiwa kifungo cha miaka kumi na mitatu jela.
Muendesha mashtaka Louis French amesema kwamba
kilo moja ya kokaine aliyokamatwa nayo Nola endapo ingefanikiwa kuiingiza
katika mitaa ya London anepata paundi laki moja na elfu themanini .kijana
aliyeambatana na Nola Raymond Goodison naye amehukumiwa kifungo cha miaka kumi
na tatu kwa kujaribu kuingiza zaidi ya kilo moja ya dawa za kulevya iana ya
kokeini .
Na inasemekana kwamba Raymond alimtumia bi
Nola kuingiza dawa za kulevya katika sidiria yake,bila wasi wasi Nola alikwenda
katika viwanja hivyo vya ndege akiwa na mtoto mdogo na ndipo alipogundulika
kuwa ameficha dawa hizo katika sidiria yake.
Williams,ni mkaazi wa Stockwell, London
kusini,amekubali makosa yake ya kusafirisha dawa za kulevya ,lakini kifungo
chake kilicheleweshwa, wakati mwanasheria wake akilalamika kuwa mteja wake
ambambikiwa kesi hiyo na kusema kuwa mwanamke huyo kosa linalomhusu ni
usafirishaji binaadamu na sio dawa za kulevya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni