Alhamisi, 5 Machi 2015

RC-NJOMBE ATANGAZA KUPAMBANA NA WAFANYABIASHARA WANAOENDELEA KUFUNGA MADUKA YAO.

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi
Na Gabriel Kilamlya  Njombe

Kitendo Cha Wafanyabiashara Kufunga Maduka Yao Kwa Kile Wanachodai ni Kuwaunga Mkono Wafanyabiashara Wenzao Akiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa Johnson Minja Pindi Anapokwenda Mahakamani Kimeikasirisha Serikali Mkoani Njombe.

Aidha Hatua Hiyo Imemfanya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi Kutoa Tamko la Kuwataka Wafanyabiashara Hao Kufungua Haraka Maduka Yao na Kuendelea na Biashara Kutokana na Athari Kubwa Zinazowakumba Wananchi.

Dokta Nchimbi Ametoa Kauli Hiyo Kufuatia Wafanyabiashara Mkoani Njombe  Kufunga Maduka Yao Hapo Machi Tatu Mwaka Huu Wakidai Wanakwenda Mahakamani Kusikiliza Kesi ya Mfanyabiashara Mwenzao Mexon Sanga na Leo Wakidai Kumuunga Mkono Mweyekiti wa JWT Johnson Minja Jambo Ambalo ni Kero Kubwa Kwa Wananchi.

Amesema Kitendo Hicho Kinasikitisha na Kinawanyima Haki Wananchi Pindi Wanapofika Dukani na Kukuta Maduka Yamefungwa Ilihali Wamekubali na Serikali Kufanyabiashara Hizo.

Kutokana na Adha Hiyo Amewataka Wafanyabiashara Hao Kufungua Maduka Yao Haraka Iwezekanavyo Huku Akiahidi Kuwachukulia Hatua Kali Wale Wote Watakaoonekana Kuwa Chanzo Cha
Wafanyabiashara Hao Kuendelea Kufunga Maduka Yao.

Hata Hivyo Amekitaka Chama Cha Wafanyabiashara Wenye Viwanda na Kilimo TCCIA Kulifikiria Kwa Kina Suala Hilo Ili Kufikia Hatima ya Kufungua Maduka Hayo Haraka Iwezekanavyo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni