Jumanne, 24 Februari 2015

Pinda azindua BVR mkoani Njombe


Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda

Na Michael Katona, Makambako

Makambako. Waziri Mkuu Mizengo Pinda jana amezindua rasmi zoezi la uandikishaji wananchi katika daftari la wapiga kura katika Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa Mkoa wa Njombe, huku akielezewa changoto kadhaa zilizolikumba zoezi hilo ikiwemo ya mashime kushindwa kutambua alama za vidole kwa baadhi ya wananchi.

Changamoto hizo zilielezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji Damian Lubuva, aliyetumia muda mwingi kuvilaumu vyombo vya habari kwa kuandika kasoro zinazojitokeza katika zoezi kuliko mafanikio.

Jaji Lubuva alisema vyombo vya habari vinatumia muda mwingi kuandika kasoro zilizojitokeza katika uandikishaji na kusema kwamba kasoro haziwezi kukosekana katika kazi yoyote duniani.


Aliongeza kuwa,mapungufu yaliyojitokeza katika BVR yasigeuzwe ni mradi kwa wanasiasa  kwa kuzungumza upungufu huo bali wasaidie kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha badala ya kuwakatisha tamaa .” iongozi wa Siasa wanasema Jaji Lubuva tunamheshimu lakini amepewa kuendesha zoezi la kihuni hii ni hukumu ambayo ninapewa ambayo  hata kama ikienda Rufaa inatupiliwa mbali, alisema Jaji Lubuva.

Aliongeza kuwa , pale inapotokea mapungufu ya Mashine tunajitahidi  kulekebisha na kuwa hakuna Mwananchi ambaye hatajitokeza na kuachwa kuandikishwa . Waziri Mkuu Mizengo Pinda amezindua zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe na kusema  mfumo mpya wa (VBR )utatumika kutatua changamoto mbalimbali zilizokuwa zikijitokeza wakati wa chaguzi zilizopita.

Pinda alisema tayari tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imefanyia marekebisho ya kasoro zote zilizokuwa katika mfumo huo ambazo zilijitokeza wakati wa zoezi la majaribio lilifanyika katika ya Desemba 15 na 24 mwaka jana.

Akifafanua zaidi Pinda alisema uboreshaji wa daftari la kudmu la wapiga kura litahusisha kuandikisha wananchi wote wenye sifa za kupiga kura  ikiwa ni wale waliojiandikisha awali,ambao hawajajiandikisha na waliopoteza vitambulisho.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi amesema kuwa zoezi la uandikishaji wa Daftari la kudumu la kupiga kura kutumia mfumo wa kieletronic BVR ambalo limeanza hii leo limepokelewa kwa muitikio mkubwa wa wananchi kwenda kujiandikisha hasa vijana.



Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt Rehema Nchimbi.
Akizungumza na East Africa Radio Dkt. Nchimbi amesema kuwa muitikio huo umetokana na uhamasishaji na uelimishaji juu ya umuhimu wa kujiandikisha katika daftari hilo ili kuweza kupata nafasi ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
Aidha Dkt. Nchimbi ameitaka Tume ya taifa ya uchaguzi NEC kujiimarisha zaidi ili zoezi hilo lisijekukumbwa na dosari kama zilizojitokeza wakati wa uandikishaji wa majaribio na kuongeza kuwa mpkaa sasa hawajapata taarifa ya usumbufu wa vifaa ila ameahidi kufuatilia suala hilo kwa ukaribu zaidi.
Dkt. Nchimbi ametoa wito kwa vijana pamoja na makundi mengine kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu kwenye zoezi hilo linalotumia mfumo wa kielektroniki wa BVR, ambao ndio utakuwa unamtambulisha rasmi mpigakura nchini.
Ameongeza kuwa uzinduzi rasmi wa zoezi hilo unatarajiwa kuzinduliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda hapo Kesho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni