Jumanne, 24 Februari 2015

VURUGU ILULA, POLISI WAKIMBIA KITUO, WANANCHI WACHOMA MOTO MAGARI


WANANCHI wenye hasira mjini Ilula, mkoani Iringa, wamevamia kituo cha polisi na kuvunja milango kisha kuwafungulia mahabusu waliokuwemo ndani, wakachoma moto baadhi ya magari yaliyokuwepo kituoni hapo pamoja na mafaili.


Inasemekana polisi walivamia eneo la kilabuni na kuanza kupiga kila raia na kusababisa kifo cha huyo mama muuza Pombe za kienyeji. 

Kosa likiwa ni kufungua kilabu cha Pombe kabla ya muda ulioruhusiwa kisheria. 

Wananchi wamechoma matairi barabara Kuu hakuna gari inayopita, Polisi bado hawajafika waliopo wamekimbia baada ya kuzidiwa na wananchi.


Gari tatu zilizosheheni FFU ziliwasili na mabomu yalipigwa mfululizo, na kusafisha  barabara kwa kuzima moto na kutoa matairi njiani. 

Wananchi Walioenda kituoni wamechoma moto matairi na magari mabovu yaliyopakiwa kituoni hapo.

Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,  limetokea leo asubuhi kufuatia mwanamke ambaye hakufahamika jina lake kujigonga ukutani na kuanguka kisha kufariki dunia wakati akiwakimbia polisi waliokuwa kwenye oparesheni ya kuwakamata watu wanaokunywa pombe wakati wa asubuhi.

Habari zaidi zinapasha kwamba, licha ya kuchoma moto magari, waliziba barabara kuu ya kwenda mikoani na kuyazuia magari kupita, hali iliyosababisha polisi kuwakabili lakini walizidiwa nguvu na kuingia ndani ya basi la Nyagawa.

Askari wakiwa ndani ya gari hilo waliendelea kushambuliwa na wananchi kwa mawe na kuvunja vioo vyake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni