Ijumaa, 6 Machi 2015

Mdau Henry Mdimu aanza harakati za kutoa somo kwa wauaji wa albino

 Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu (kati) azungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati azungumzia harakati zake za kutaka kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.Kulia ni Mwenyekiti wa Imetosha Movment,Masoud Ali "Kipanya" na kushoto ni Monica Joseph mjumbe wa Imetosha.
 Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni Wajumbe wa Imetosha,Joachim Mushi akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo.
Baadhi ya Wajumbe wa Imetosha wakiwa kwenye picha ya pamoja.


Na Chalila Kibuda 

Balozi wa Imetosha,Henry Mdimu amewataka watu wajitokeze katika  harakati za kupambana na watu wenye imani  potofu za kuwaua watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino).

Mdimu amesema uchunguzi umebaini ukosefu wa elimu kwa watu wenye imani hizo ndiyo hupelekea mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hivyo silaha ya elimu ni sehemu kubwa ya harakati hapa nchini.

Hayo ameyasema leo wakati alipokutana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam na kusema kuwa ana mpango wa kwenda kanda ya Ziwa ili kuihamasisha  jamii juu ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Aidha,Mdimu ameahidi kutoa elimu hiyo kwa njia ya sanaa kwa kuwatumia baadhi ya wasanii kama Jhikoman,Kassim Mganga,Profesa J,Ray C,Fid Q,Roma Mkatoliki pamoja na Dami Msimamo.

Pia amevitaka Vyombo vya Habari kutoa ushirikiano katika harakati hizo za  kuhakikisha wanatokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
    Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akitoa hotuba wakati akifungua semina kwa ajili ya Maafisa Rasilimali watu Mkoa wa Mbeya iliyoandaliwa na mfuko wa hifadhi ya jamii wa GEPF.


  Meneja Biashara wa GEPF Taifa, Aloyce Ntukamazina akitoa taarifa ya mfuko la lengo la Semina kwa washiriki wa semina hiyo.

Meneja Biashara wa GEPF Taifa, Aloyce Ntukamazina akitoa mada katika semina kwa Maafisa Rasilimali watu Mkoa wa Mbeya.

Washiriki wa semina wakisikiliza mada zinazowasilishwa kuhusiana na mfuko wa GEPF.



Washiriki wa Semina wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya.



MKUU wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka wananchi wote kujenga utamaduni wa kujiunga na mifuko ya hifadhi za jamii kwa ajili ya manufaa ya uzeeni na kupunguza malalamiko.

Kandoro alitoa wito huo  alipokuwa akifungua semina kwa ajili ya Maafisa rasilimali watu wa Mkoa wa Mbeya iliyoandaliwa na Mfuko wa pensheni wa GEPF, iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill view Uzunguni jijini hapa.

Alisema kuna dhana iliyojengeka miongoni mwa jamii kuhusu mifuko ya hifadhi za jamii kuwa ipo kwa ajili ya waajiriwa wa serikali tu jambo ambalo ni kinyume kwani kila Mtu ana haki ya kujiunga na mfuko wowote anaoutaka kwa ajili ya manufaa ya baadaye.

Alisema mifuko hiyo ipo kwa ajili ya uwekaji wa akiba kwa hiari kwa mwajiriwa wa serikali na aliyejiajiri mwenyewe kama Mkulima, Mfanyabiashara,mfugaji, machinga, madereva wa bodaboda, bajaji na wajasiliamali wadogo ambao kwa mujibu wa sera wanapaswa kujiunga bure.

Aidha alitoa wito kwa wenye mifuko kuhakikisha inaendesha mambo yake kwa uwazi na kuimarisha mfumo wa Tehama ili utoaji taarifa kwa wanachama uwe sahihi na kwa wakati wote.

Aliongeza kuwa mifuko hususani GEPF iwe na utaratibu wa kuwafuatilia wanachama wake kuhakikisha michango inafika kwa wakati na sio kukaa maofisini kusubiria mwajiri kupeleka ili hali kuna wengine hawapeleki makato ya waajiriwa wao jambo ambalo litasaidia kuondoa migogoro isiyokuwa ya lazima.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Meneja Masoko wa GEPF taifa,Aloyce Ntukamazina, alisema sababu ya kuendesha semina hiyo kwa Maafisa rasilimali watu wa Mkoa wa Mbeya ni kutokana na wao kuwa ndiyo washauri na waajiri wa watumishi wageni.

Aliongeza kuwa sababu nyingine ni kuza Mfuko huo Mbeya, mabadiliko makubwa ya mifuko nchini hivyo kuwa na umuhimu wa kutoa semina elekezi kwa wadau ambao ndiyo waajiri wakubwa.

Alisema pia kuna mabadiliko makubwa ya kimfumo katika mfuko wa GEPF pamoja na ongezeko la mafao ambapo pia Afisa rasilimali watu ni kiungo kikuu kati ya Mwajiri, mwajiriwa na Mfuko hivyo kuona umuhimu wa kuwaelimisha wao ili waweze kutoa ushauri kwa vijana ambao hawajajiunga na mfuko wowote.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni