Hatimaye wakurugenzi wa Mashauzi Classic na Jahazi Modern Taarab, wamefanya mkutano na waandishi wa habari na kuthibitisha kuwepo kwa onyesho la pamoja la makundi hayo yenye nguvu katika muziki wa taarab.
Onyesho hilo litafanyika Jumapili, Machi 22, mwaka huu, ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Jahazi, Mzee Yussuf na Mkurugenzi wa Mashauzi Classic, Isha Ramadhani maarufu kama Isha Mashauzi, wamesema siku hiyo hatumwi mtoto dukani.
Wakiongea katika mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika Jumatatu iliyopita katika hotel ya Travertine, wakurugenzi hao, ambao wote ni waimbaji nyota, walisema onyesho hilo si mpambano,
bali si la masihara kwani kila bendi imejipanga kuhakikisha inaangusha burudani iliyokwenda shule
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni