IGP Mangu alitoa ufafanuzi huo jana wakati akizungumza na gazeti hili baada ya kuwapo malalamiko kutoka kwa baadhi ya askari wa jeshi hilo kupandishwa vyeo, huku mishahara yao ikiendelea kubaki kama ilivyokuwa zamani.
“Nimezunguka nchi nzima na kuzungumza na askari kuhusu jambo hili,” alisema Mangu.
Katika taarifa ambazo gazeti hili ilizipata, kuna baadhi ya askari wamepandishwa vyeo na kudumu navyo hadi miaka miwili sasa, lakini bila kurekebishiwa viwango vya mishahara.
Mmoja wa askari aliyezungumza na gazeti hili (jina linahifadhiwa) alisema: “Nimepandishwa cheo miaka miwili sasa, lakini jambo la kushangaza hadi leo mshahara wangu haujarekebishwa. Kwa namna moja au nyingine, suala hili lina athari kwani unaonekana una cheo kikubwa, lakini kiuchumi bado uko vilevile.”
Wengi wa askari wenye matatizo hayo ni wale waliopandishwa kutoka NCO (askari wasio na kamisheni) na kupewa kamisheni (Inspekta Msaidizi wa Polisi), ambao masilahi yao hutofautiana ili kukidhi hadhi za vyeo hivyo.
IGP Mangu alifafanua kwa kusema: “Askari wote wanajua kinachoendelea, kama kuna mwenye dukuduku lolote utaratibu wa kupata taarifa upo wazi ndani ya jeshi.”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni