Jumanne, 11 Novemba 2014

NYALANDU ALIA NA SHERIA ZA UJANGILI ZILIZOPO SASA



Lazaro Nyalandu, Waziri wa Maliasili na Utalii


Na Mwandishi Wetu, BrotherDanny Blog


Arusha: WIZARA ya maliasili na utalii inatarajia kupitia Sheria zote za makosa dhidi ya wanayama pori kwa lengo la kufanyia maboresho Sheria za adhabu kwa watuhumiwa wa makosa ya ujangili.

Hayo yalisemwa jana na Waziri wa Wizara hiyo,Lazaro Nyalandu wakati alipokuw akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC) uliokuwa unafanyika jijini Arusha.
Aidha katika mkutano huo uliokuwa unajadili  mbinu za kupambana na uhalifu dhidi ya wanyamapori,Nayalandu alisema kuwa watapitia Sheria hizo kwa lengo la kuongeza adhabu kwa watuhumiwa wa vitendo vya ujangili.

“Siridhishwi na Sheri za sasa hivi kwani  adhabu zinazotolewa kwa watuhumiwa wa ujangili ni ndogo ila Wizara tunatarajia kupitia Sheria zote zinazohusu makosa dhidi ya wanayamapori  kwa lengo la kuweza kuangalia namna ya kuongeza adhabu,” alisema.

Alisema kuwa hadi hivi sasa silaha zaidi ya 3000 zinazotumika katika vitendo vya ujangili ikiwemo sihala za kivita kama vile AK 47 na Gobore,zimeweza kukamatwa na kwa kipindi cha Mwaka 2013 watuhumiwa 1816 walikamatwa na kesi zao zinaendelea katika Mahakama mbalimbali hapa nchini.

Aidha katika Mkutano huo pia watajadili  mbinu na njia ambazo zitakuwa ni shirikishi za nchi kwa pamoja za kuweza kupambana na uhalifu dhidi ya wanyamapori,kutafuta njia na mipango inayosadikika ya kuweza kuzuia utoroshwaji wa  wanyama nje ya nchi na kusimamia ulinzi wa mipaka.

Awali Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Mazingira,James Lembeli,aliitaka Serikali bila kuangalia nafasi ya mtuhumiwa aliyo nayo,kuwachukulia hatua kali za kisheria pamoja na kufanya marekebisho ya adhabu kwa watuhumiwa.

“Suala la ujangili limekuwa ni tatizo kubwa  katika nchi yetu, Tanzania tuna mipango na mikakati tunayo mizuri  lakini watuhumiwa wa ujangili wafiksihwe Mahakamani ili tuone jitihada za Serikali na adhabu kali zitolewe kwani kumekuwa na matukio na matukio ya kukamata watu lakini kesi hizo hatuzisikii.”


Alisema kuwa ili  mapambano ya ujangili liweze kufanikiwa ni lazima watuhumiwa  bila kujali nafasi zao, wala ,nchi wanazotoka,wakikamatwa hapa nchini wafikishwe kwenye vyombo vya  dola  na adhabu kali zitolewe.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni