Jumapili, 2 Novemba 2014

MWANAMKE AISHI KINYUMBA NA WANAUME WAWILI KWA MIAKA NANE BILA KUTAMBUANA MBEYA

 Juliana Josia(22)kushoto anaedaiwa kuishi na wanaume wanaume wawili kwa zaidi ya miaka 8 bila kutambuana akiwa na Mume wake halisi Rogers ofisini kwa mtendaji


 Juliana Josia(22)kushoto akiwa na barozi Dinde 

Bwana Rogers akiongozana na baadhi ya viongozi wa mtaa kwenda kituo cha polisi


Mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Juliana Josia(22)amezua utata hivi karibuni baada ya kugunduliwa akishi na wanaume wawili kwa muda wa miaka minane bila wanaume hao wawili  kujitambua.

Hayo yalibainika katika kituo cha Polisi Kati Jijini Mbeya baada ya Mwanamke huyo kudai kuporwa mtoto mgogoni jinsi ya kike mwenye umri wa miaka miwili eneo la Mwanjelwa Jijini Mbeya baada ya kutishiwa na Biton Bomani Mwashilindi mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.

Juliana alidai kuporwa mtoto na Biton Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi alipokuwa akielekea soko la Sido kwenye shughuli zake za biashara na kutoa taarifa kituo cha Polisi Mwanjelwa na baadaye kituo kikuu kati na kufunguliwa jalada la wizi wa mtoto namba MB/RB/9384/2014 ambapo juhudi za kumtafuta zilifanikiwa baada ya taarifa kutolewa Kituo cha Radio cha Bomba FM Mbeya ndipo alipojisalimisha mwenyewe akiwa na mtoto Zalida Rogers(2).

Hata hivyo katika hali ya mshangao Biton alifika katika kituo cha Polisi Kati akiwa na Cheti cha kuzaliwa na kadi ya kliniki ambapo kinaonesha mtoto Zalida kuzaliwa kituo cha Afya Ruanda Mwanjelwa na kuonesha kuzaliwa 18/08/2012 wazazi wakiwa ni Juliana Josia na Biton Mwashilindi.

Biton alidai mbele ya Dawati la Jinsia la Jeshi la Polisi kuwa Juliana ni mpenzi wake kwa muda wa miaka nane na kwamba walikuwa wakikutana katika nyumba ya kulala wageni kila alipomhitaji na walikuwa wakipanga katika nyumba hiyo kwa siku saba kila wanapokutana hali ilyofanya watu wanaosikiliza tukio hilo kituo cha Polisi kushikwa na butwaa akiwemo mume halali Rogers Halinga na mke wa Biton ambaye alimtunza mtoto kwa siku nne.

Akijieleza kwa kujiamini Biton alidai kuwa hata mtaji wa biashara alimpatia yeye na hata wazazi wake Biton walioko Itaka Mbozi walimtambua mtoto Zalida na kwamba jina la mtoto alipewa na ndugu zake na hata aliowahi kuugua alikwenda Itaka Mbozi na kukaa kwa wazazi wa Biton kwa zaidi ya juma moja.

Kwa upande wa Rogers yeye alisema mtoto Zalida ni wa kwake na kwamba aliondoka kwao akiwana na ujauzito wa miezi mitano na kwamba yeye alijua kukorofishana kwao kulitokana na hali ya ujauzito na alikaa  kwamba mkewe Juliana alikaa kwao kwa miezi sita na alipojifungua alirejea kwake na aliohitaji kupata maendeleo ya mtoto mkewe alidai kuwa kadi ya kliniki imepotea.

Kikao hicho kilichokuwa na mvutano mkubwa kiliahirishwa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Mbeya kwa kumshikilia Biton kwa kosa la kutorosha mtoto na kesi ya ugoni na kuwa atafikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika huku Rogers akikabidhiwa mkewe na mtoto kwa minjili ya kwenda kuyajenga huko nyumbani kwao Kijiji cha Ishungu Kata ya Ruiwa wilaya ya Mbarali.

Baba mzazi wa Rogers Mzee Jason Halinga alisema alishangazwa na kitendo kilichofanwya na mwanamke huyo ambapo alidai kuwa mwanae alioa kihalali na kufuata mila zote na kulipa mahari lakini alishangazwa na kitendo cha wazazi wa Juliana kushindwa kuonesha ushirikiano hali inayoashiria kujua kile kilichokuwa kinafanywa na mtoto wao.

Biton alifika kituo cha Polisi akiwa na mkewe wa ndoa ambapo naye hakufahamu kuwa mumewe anaishi na mke mwingine nje ya ndoa na kwamba mtoto Zalida alipoletwa kwake hakuambiwa chochote kile na kwamba ameishi kwenye mateso ya ndoa kwa muda wa miaka nane huku akifanyiwa vitendo vya kikatili na mumewe ikwa pamoja na kuambulia kipigo mara kwa mara.

Baadhi ya ndugu wa Rogers walioneshwa kukerwa na baadhi ya Askari wa ngazi  juu katika Dawati la Jinsia Kituoni hapo ambao walonesha kutojali suala hili huku wakitioa maneno ya kejeli hali inayotia dosari utendaji kazi wa Dawati hilo na kwamba lipo kibiashara zaidi na si  huduma kama ilivyo sera ya Jeshi la Polisi.

Hata hivyo hawakusita kuwapongeza Askari wa Kiume walionesha juhudi hata kufanikwa kupatikana kwa mtoto Zalida na Biton pamoja na rafiki yake.

Katika sakata hili kama si juhudi za Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi kuingila kati basi mtoto Zalida asingeweza kupatikana kama baadhi ya watoto waliotoweka maeneo mbalimbali Mkoani Mbeya ambao hawajapatikana mpaka sasa ambapo wananchi wamelalamikia Kituo Kikuu cha Kati kwa kutochukua hatua za haraka za kukomesha vitendo vya ukatili wa Kijinsia na baadhi kuamua kumalizana wenyewe mitaani vikiwemo vitendo vya ubakaji ambavyo vimeshamiri mkoani Mbeya.

Hatima ya ndoa ya Rogers na Juliana itajulikana baada ya mazungumzo yatayofanyika kwa Mzee Jason Halinga nyumbani kwake Ishungu Kata ya Ruiwa hivi karibuni kikao kitakutaniha pande mbili za wazai ili kufikia muafaka katika sakata la aina yake na kwamba hata kubainika kwa sula hili ni kutokana na Juliana kufumwa na mwanaume mwingine katika chumba ambacho Biton alikuwa awe na Juliana ndipo alipoamua kulipiza kisasi kwa kutorosha mtoto.

Na Mbeya yetu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni