Kikosi cha Taifa Stars kitakachokuwa na mabadiliko mengi
Na Mwandishi Wetu
MWAMUZI wa FIFA, Hakizimana Louis
kutoka Rwanda ndiye atakayepuliza filimbi katika mechi baina ya Taifa Stars na
Benin itakayochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili,
Oktoba 12, mwaka huu.
Hakizimana atasaidiwa na Wanyarwanda
wenzake Simba Honore na Niyitegeka Jean Bosco.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mechi hiyo itaanza kuchezwa saa 11 jioni.
"Mechi hiyo itatanguliwa na ile
ya viongozi wa dini - Waislamu vs Wakristo kudumumisha upendo, amani na
ushirikiano itakayoanza saa 9 kamili alasiri. Tiketi za elektroniki
zitakazotumika kwa mechi hiyo tayari zimeanza kuuzwa kwa kiingilio cha Sh. 4,000
na Sh. 10,000," imesema taarifa hiyo iliyotolewa muda mfupi uliopita.
Wakati huo huo, Kocha wa Stars, Mart
Nooij, ameongeza wachezaji watatu kwenye kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager ili kukiongezea nguvu kwa ajili ya mechi
hiyo.
Wachezaji walioongezwa ni Jonas Mkude
na Joram Mgeveke kutoka timu ya Simba, na Gadiel Michael wa Azam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni