Na Mwandishi Wetu
MWIMBAJI nguli wa muziki wa
Injili Tanzania, John Lisu juzi alikonga nyoyo za mamia ya wadau waliojitokeza
katika uzinduzi wa albamu yake ya Uko Hapa yenye nyimbo 18, uliofanyika katika
Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Uzinduzi huo uliofanyika mbele ya
mgeni rasmi, Waziri wa Waziri Nchi Ofisi ya Rais-Mahusiano na Uratibu, Stephn
Wassira, ulikuwa na mvuto mkubwa sio tu kutokana na umahiri wa mwimbaji huyo,
pia maandalizi yaliyofanywa na wadhamini.
Lisu alipopanda jukwaani, alifanya
kweli kwa kuimba nyimbo zaidi ya tano zilizopo katika albamu hiyo
iliyozinduliwa.
Lisu aliyepanda jukwaani saa 12
jioni, alidhihirisha uwezo wake wa kushambulia jukwaa kwa kuimba hadi saa mbili
bila kuonesha kuchoka.
Uzinduzi wa albamu hiyo uliofanywa na
Waziri Wasira, iliwekwa baraka baada ya kuzinduliwa na maaskofu
watano wa Makanisa tofauti.
Hao ni Askofu Lawrance Kametta
(TAG-Jimbo la Mashariki), Askofu Deo Rubala (Word Alive Centre), Askofu Bruno
Mwakibolwa, Mtume Peter Nyaga (RGC-Miracle Centre) na Machungaji Paul Safari
(DPC).
Lisu alilitumia jukwaa hilo
lililolipuka kwa shangwe za mashabiki alipoimba na mkewe, Nelly wimbo wake mpya
wa Mfalme ambao unatarajia kuwemo katika albamu yake mpya ambayo ipo katika
maandalizi.
Aidha, Lisu kabla ya kuimba na mke
wake (Nelly), alitumia jukwaa hilo kuwatambulisha watoto wake mapacha na
kuwabariki ambako pia alitoa ushuhuda baadaye watakuwa wachungaji.
Pia, jukwaani aliimba mojawapo ya
nyimbo zake na muimbaji kutoka Kenya, Timoth Kaberia. Aidha, Lisu alitumia
fursa hito kutoa shukrani kwa waliofanikisha safari yake ya muziki huo.
DVD hizo zilizozinduliwa ambazo idadi
yake ni 18 zimegawanyika sehemu mbili ni pamoja na Wakusifiwa,
Wastahili sifa, uko juu, Inuka, Uko Hapa, Nijaze, Nitaongozwa, Wastahili Bwana,
Roho Mtakatifu na Mtakatifu.
Nyingine ni Yu Hai Jehovah,
Atikisa, Upendo Upendo, Mataifa Yakujue, Umejawa na Ukuu, Fungua Macho,
Haleluya naMungu Ibariki.
Naye Mkurugenzi wa Msama Promotions
ambao ni wadhamini wa uzinduzi huo, Alex Msama, alishukuru mapendekezo ya
mabadiliko yaliyopendekezwa katika Katiba mpya ambayo yanawatambua wasanii.
Alisema kutambulika huko kumetokana
na mshikamano uliopo katika ya wasanii na serikali hivyo alitoa wito kwa
wasanii kuongeza jitihada za ufanikishaji wa kazi zao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni