Na Mwandishi Wetu
Ngorongoro: Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro(NCAA)imefanikiwa kutoa ng'ombe 20 wa kisasa wenye thamani ya zaidi
ya milioni 20 kwa vijiji vinne vya Wilaya ya Karatu kwa madhumuni ya kuendeleza
Uhifadhi wa maliasili ndani ya Vijiji hivyo.
Akiongea na waandishi wa habari
mapema wiki hii Afisa Ugani wa Mamlaka hiyo ambaye ni Bw Salustin Hallu alisema
kuwa huo ni moja ya miradi inayotekelezwa na mamlaka hiyo.
Alisema kuwa mradi huo ambao hapo
awali ulianza rasmi na ng'ombe wa kisasa 20 uliweza kuwa na manufaa makubwa
sana kwa Vijiji vya Troma, Ayalabe, lositete na Upperutele ambapo hapo awali
baadhi ya wafugaji kwenye vijiji hivyo walikuwa wanalazimika kuchunga ndani ya
hifadhi
Alifaafanua kuwa mpaka sasa zaidi ya
familia 98 kwenye mradi huo tayari wameshanufaika kwa kuwa kila familia moja
sasa ina ng'ombe wa kisasa mmoja na lengo halisi likiwa ni kuhakikisha kuwa
kila familia inajijengea uwezo wa kuchunga ndani na wala sio kutoa mifugo
kwenda kutafuta malisho nje.
“Ngorongoro inalinda sana ujirani
mwema na wananchi wake na ndio maana tukaona kuwa badala ya kuwakataza tu
wananchi wasiingie kwenye pori ambapo ni hatari kwa maisha yao wao pamoja na
mifugo lakini pia tuwape mbinu mbadala za kuhakikisha kuwa wanajikomboa ndio
maana tukaanzisha huu mpango ambao umeonekana kuwasaida sana wananchi wa hivi
vijiji,” aliongeza Hallu.
Awali alisema Mamlaka pia bado ina
mkakati mbalimbali wa kuhakikisha kuwa wanaweza kufikia familia zote sanjari na
kuwapa elimu mbalimbali juu ya umuhimu wa kufuga ndani laki ni pia kuwapa mbinu
imara ambazo zinatakiwa kutumiwa na wafugaji wa kisasa zaidi.
Akiongea kwa niaba ya familia 98
ambazo zimenufaika na mradi huo wa ngombe wa kisasa kutoka Mamlaka ya hifadhi
ya Ngorongoro bi Emirita Martin alidai kuwa pamoja na kuwa wamepata ng'ombe
lakini bado Mradi huo unapaswa kuongezewa ngombe ambao wataweza kuwanufaisha
wanawake.
Bi Emirita alibainisha kuwa kama kila
Boma na familia zitapata ng'ombe mmoja ambaye atazaliana basi wakina mama
wataondokana na dhana ya kuwa tegemezi kwenye maisha ya kifamilia kwani ufugaji
unabadilisha maisha duni na maskini ambayo wanayo baadhi ya wanawake katika
Wilaya hiyo ya Karatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni