Jumanne, 7 Oktoba 2014

RAIS JK AMTEUA MKUU MPYA WA MASHITAKA (DPP)


Rais Dk. Jakaya Kikwete

Rais wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Biswalo Mganga kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) nchini.


Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar Es Salaam, leo, Jumatatu, Oktoba 6, 2014, na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi (KMK), Bwana Peter Ilomo imesema kuwa uteuzi huo umeanza Ijumaa iliyopita, Oktoba 3, mwaka huu, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mganga alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka na Wakili wa Serikali Mfawidhi.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu – Dar es Salaam. 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni