Jumatatu, 6 Oktoba 2014

WAKAZI WA DODOMA WASAMBAZA UPENDO WA KUTOSHA NDANI YA TAMASHA LA FIESTA MKOANI DODOMA



Msanii wa bongofleva kutoka kampuni ya No Fake Zone Lina Sanga akiimba wimbo wake wa Ole Temba ambao umepokelewa vyema na mashabiki wake, ndani ya tamasha la Fiesta lililofanyika usiku wa kuamkia leo ndani ya uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.

 Pichani ni kulia ni Msanii wa bongofleva Abdul Kiba akiimba sambamba na kaka yake Alli Kiba ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga ya muziki wa kizazi kipya kupitia nyimbo zake mbili alizoziachai hivi karibuni, ikiwemo Mwana Daisalama na Kimasomaso.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka THT, Rachael akitumbuiza jukwaani pamoja na mcheza shoo wake mbele ya mashabiki wa tamasha la Fiesta 2014 lililofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri, mkoani Dodoma usiku wa kumkia leo.




Hakuna maoni:

Chapisha Maoni