Mwenyekiti wa kamati ya harambee ya kuichangia radio Maria mkoa wa Iringa Paschal Bella kushoto akimpongeza mbunge wa jimbo la Kalenga, Godfrey Mgimwa kwa kuichangia radio Maria Tsh milioni 1.5 alipokuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo.
Mbunge Mgimwa akipongezwa baada ya kuchangia milioni 1.5 radio Maria
Na Mwandishi Wetu
VYOMBO vya habari
zatakiwa kuepuka kupotosha umma juu ya mchakato
mzima wa bunge la katiba lililomalizika jana mjini
Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa
leo katika viwanja vya kanisa la Rc Mshindo na mbunge wa
jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa wakati akichangia kiasi
cha Tsh milioni 1.5 wakati wa harambee ya kuichangia
radio Maria.
Alisema kuwa iwapo
vyombo vya habari zitatumika vibaya kuna
uwezekano wa Taifa kuingia katika machafuko kama zilizo
nje nyingine na kama vyombo vya habari vitafanya kazi
yake kwa kuzingatia misingi ya maadili jamii itaunganishwa na
vyombo hivyo.
“Radio Maria ni moja kati ya
radio ambazo nimekuwa nikizifuatilia toka nikiwa mdogo
na nimekuwa nikipenda zaidi jinsi radio hiyo
inavyofanya shughuli zake na mbali ya kufanya kazi
ya kueneza injili bado imekuwa msaada mkubwa
katika kuelimisha umma……. Hivyo rai yangu kwa radio
maria ni kuona inaendelea hivyo hivyo na
ikiwezekana kuandaa vipindi kwa ajili ya elimu kwa umma juu ya
katiba mpya.”
Alisema kuwa wajumbe wa
bunge la katiba wametimiza kazi yao ambayo umma
ulitegemea kutoka kwa wajumbe hao hivyo
kazi iliyobaki ni ya wananchi kucha kuipitisha
katiba hiyo mwaka 2016 na kuwa kwa wakati huu ni vema
vyombo vya habari kuendelea kutoa elimu kwa umma
juu ya kazi nzuri iliyofanywa na bunge hilo la katiba.
Hata hivyo alisema ni
vema watanzania kuepukana na watu wachache
wasiolitakia mema Taifa ambao wanataka kuona nchi
haitawaliki kwa kutaka maandamano yasio na tija kwa jamii.
Mgimwa alisema kuwa njia
pekee ya kuepukana na viongozi wasio litakia
mema taifa ni pale ambapo vyombo vya habari
vitakapoweka msimamo wa uzalendo kwa kuepuka kuwa sehemu ya
kuhamasisha kuvunjika kwa amani nchini.
Kwa upande wake
mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harambee hiyo
Bw Pascal Bella akishukuru kwa mchango huo
wa mbunge Mgimwa alisema kuwa mbali ya kuwa
mbunge huyo ni wa jimbo la kalenga ila amekuwa
msaada mkubwa kwa kufanikisha zoezi hilo la kuichangia radio hiyo.
Bella alisema kuwa
kila mwaka na kila wakati wadau wa Radio
maria wamekuwa na utaratibu wa kuichangia radio
hiyo ambayo uendeshaji wake unategemea michango
kutoka kwa wadau mbali mbali na kuwa kwa mwaka huu mkoa
wa Iringa pekee unataraji kuchangia zaidi ya Tsh milioni 30
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni