Na Mwandishi Wetu
Arusha: SHULE za sekondari zimetakiwa kuanzisha masomo ya ujasiriamali mashuleni ili kuwawezesha wanafunzi wanapohitimu elimu yao kuweza kujiajiri wenyewe badala ya kusubiria ajira kutoka serikalini.
Aidha baadhi ya vijana wamekuwa wakikosa mbinu za kujiendeleza kimaisha kutokana na wao kukosa elimu ya ujasiriamali hivyo kuwafanya washindwe kufikia malengo yao kutokana na wao kusubiria ajira tu badala ya kujiajiri wenyewe.
Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa shule ya Wining Spirit sekondari Maxmillian Iranqhe alipokuwa akizungumza na walezi pamoja na wadau wa elimu katika mahafali ya sita kidato cha nne ambapo jumla ya wahitimu 72 walitunukiwa vyeti vyao.
Iranqhe alisema kuwa ili kuwwezesha vijana waweze kupambana na changamoto ya ajira za serikalini shule za sekondari zinapaswa kunzisha mfumo wa masomo ya ujasiriamali mashuleni ili pindi wanapokosa ajira waweze kujiajiri wenyewe kwa kujitengenezea bidhaa mbali mbali kutokana na elimu hiyo.
Alieleza kuwa endapo wanafunzi wataweza kupata elimu ya ujasiriamali itaweza hata kuisaidia serikali kutengeneza ajira kwa kuwa wengi wao watajiendelez nayo na hivyo kupunguza tatizo la ajira serikalini.
“hapa shuleni mimi nimeanzisha utaratibu maalum wa kufundisha msomo ya ujasiariamali na huu mpango unasaidia sana kwa kiwango kikubwa kkuwasaidia vijana waweze kujiajiri wenyewe kwa kupitia elimu hii kuliko pale ambapo vijana wanahitimu na hawana elimu ingine ya ziada jambo ambalo linawafanya waone maisha ni magumu," aliongeza.
Alifafanua kuwa ili kuhakikisha kuwa vijana wanaohitimu kidato cha nne wanajiajiri wenyewe shule hiyo ina mkakati wa kuendeleza shule hiyyo iweze kuwa na chuo cha ufundi na ujasiriamali ili kiweze kunufaisha vijana wanaomaliza elimu ya sekondari.
Awali mgeni rasmi katika mahafali hayo ambaye ni meneja wa kituo cha biashara benki y nmb Jonathan Kombe aliwataka wahitimu hao kutojiona wamemliza elimu badala yake watumie elimu ya ujasiriamali waliiyoipata kujiendeleza ili kupunguza tatizo la ajira ambalo linaikabili serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni