Audrey
amekuwa akitaka baraza la mitihani kubadili jina lake na utambulisho wake wa
kijinsia
Mwanamke aliyebadili jinsia yake ya kiume na kuwa mwanamke
na kutaka jina lake kubadilishwa kwenye cheti chake cha mtihani ameshinda kesi
yake dhidi ya baraza la kitaifa la mitihani nchini Kenya.
Mahakama imelazimisha baraza hilo kumpa Adrey Mbugua cheti
kipya kinachoonyesha hali yake mpya ya kijinsia hasa kwa kuwa anapokea matibabu
ya kufanikisha jinsia yake kubadilika kabisa.
Bi Mbugua alilishitaki baraza la kitaifa la mitihani
nchini humo kwa kukataa kubadililisha utambulisho wa jinsia yake kwenye cheti
hicho kutoka kwa Mwanamme na kumtambua kama mwanamke licha ya amri iliyotolewa
katika gazeti rasmi la serikali.
Jaji Weldon Korir amelipatia baraza hilo hadi siku 45
kubadilisha jina la Adrey katika cheti hicho kutoka kwa 'Andrew Mbugua' na
utambulisho wa mwanamume na kulibadilisha kuwa jina la kike la 'Audrey Mbugua'
bila ya kuweka jinsia yoyote.
Jaji alisema kuwa jinsia ya Adrey kwenye cheti hicho
haiongezi thamani yoyote kwa matokeo yake wala alama alizopata Audrey na
kuondolewa kwake vile vile hakuna athari yoyote.
Aliongeza kuwa Audrey ameonyesha kuwa yuko tofauti na
hivyo ndivyo anavyopaswa kutambuliwa.
'Audrey ni mwanadamu ambaye anajitambua kwama mwanamke wala
sio kama mwanamume jinsia aliyozaliwa nayo,'' alisema jaji.
Jaji alisema kuwa katiba ya nchi inaamrisha watu
kuwaheshimu wengine kama ipasavyo bila ubaguzi wowote na kwamba heshima hiyo
inahusu mambo mengi ikiwemo mtu anavyotaka kutambuliwa.
Aliongeza kuwa ili Audrey kuhisi kuwa sawa anapaswa
kukubalika kama alivyo na kumyima haki hiyo ya kubadilisha jina lake katika
chati chake itakuwa ukiukwaji wa haki zake za kibinadamu.
Wakili wa Audrey, aliambia mahakama kuwa mteja wake
alizaliwa na kasoro ya kijinsia na kwamba anaendelea kupokea matibabu.
CREDIT: BBC/SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni