Kikosi cha Coastal Union
NA
MWANDISHI WETU, TANGA
UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga
umesema utakwenda mahakamani kuishtaki Kampuni ya Binslum Tyre kutokana na
kitendo cha kutengeneza T-Shirt za Coastal Union zenye nembo ya kampuni ya
Sound na kuwapa bure mashabiki kuingia nazo kwenye mechi mbalimbali za Ligi Kuu
Tanzania Bara wakiwa wamelipiwa na viingilo vya mchezo husika.
Hali hiyo ni kinyume na utaratibu kutokana na
kuwa tayari kampuni hiyo ilishajitoka kufadhili timu hiyo na tayari klabu ya
Coastal Union ilikwishapata mfadhili mwengine ambayo ni kiwanda cha Kutengeneza
Unga Ngano mkoani Tanga cha Pembe Flours Mills.
Kauli hiyo imetolewa kwenye kikao cha Kamati ya
Utendaji Kilichoketi mwishoni mwa wiki ambapo kilikuwa na agenda nne za msingi
ambazo ni Suala la mshambuliaji wa Coastal Union Danny Lyanga,Utoaji slipi
benki,Jezi za Sound,Tarehe ya Uchaguzi.
Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi wa
mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal
Union,Steven Mguto,Katibu Mkuu Kassim El
Siagi,Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Albert Peter Saimu Amiri na Meneja wa
Coastal Union Akida Machai.
Kimsingi suala ambalo lilikuwa gumzo ni suala la
kampuni hiyo kuchukua hatua ya kuwavalisha mahsbiki wa Coastal Union jezi
pamoja na kuwalipia viingilio vya mechi kwenye mechi mbalimbali za ligi kuu.
Kama unavyojua kuwa Kampuni ya Binslum Tyres
ilikuwa mhisani wetu na sasa hatuko naye na tayari alishapeleka fedha zake
kwenye vilabu vingine ikiwemo Mbeya City sasa tunamshangaa kuendelea kufanya
biashara ya matangazo kupitia mashabiki wetu kwa kuwapa tisheti za kuvaa bure
ikiwemo kuwalipia viingilio kwenye mechi za ligi kuu zinazochezwa Mkwakwani.
Hivyo kutokana na suala hilo tayari uongozi wa
Coastal Union umeshamkamata mshabiki mmoja ambaye ni wakala wa kusambaza
tisheti hizo kwa mashabiki na kumpeleka polisi na taratibu za kisheria
zinaendelea ili kuweza kukomesha vitendo hivyo ambavyo sio vya kiungwana.
Tayari Kampuni ya Pembe Flours Mills ilishasaini
mkataba na Klabu ya Coastal Union wa kufadhili kwa kipindi cha mwaka mmoja
hivyo Kampuni hiyo kuendelea kufanya matangazo yake kupitia mashabiki hao ni
kuvunja utaratibu uliokuwepo.
Hata hivyo tayari Pembe walishatoa jezi 2000 kwa
ajili ya kuziuza kwa masabiki mbalimbali wa soka jijini Tanga zilizokuwa na
nembo ya pembe na TSN.
Kuhusu suala la Uchaguzi wajumbe wa Kamati hiyo
walikubaliana uchaguzi huo ufanyika Novemba 23 mwaka huu ambapo nafasi
zitakazojazwa ni Mwenyekiti wa Klabu hiyo na wajumbe wawili wa kamati ya
utendaji
Suala la Utiliaji Sahihi wajumbe walilipendekeza
fedha zitumike kwenye matumizi yanayofahamika ikiwemo kuwekwa utaratibu wa wazi
kwenye matumizi husika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni