Na Woinde Shizza, Arusha.
Kiongozi wa matukio ya ulipuaji wa mabomu na umwagiaji
tindikali viongozi wa dini aliyejulikana kwa jina la Yahaya Hassani Omary
ameuwawa na jeshi la polisi wakati alivyokuwa akijaribu kukimbia.
Akithitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani
Arusha,SACP Liberatus Sabas (pichani) Alisema kuwa tukio hilo limetokea
October 19 majira ya saa tano na nusu katika barabara ya babati
mkoani Arusha wakati alipokuwa akijaribu kuwakimbia polisi.
Alisema kuwa mtuhumiwa huyo wa ugaidi alishikiliwa wiki
mbili zilizopita huko mkoani Morogoro mara baada ya kutafutwa kwa
muda mrefu na hapo jana alikuwa akipelekwa wilayani kondoa mkoani Dodoma
kwa ajili ya kwenda kuonyesha sehemu ambazo alikuwa ameficha mabomu
mengine.
"mtuhumiwa huyo alikuwa anasakwa kwa muda mrefu bila
mafanikio kwani alikuwa hakai sehemu moja ila jeshi la polisi huko mkoani
morogoro lilimkamata wiki mbili zilizopita na baada ya kufanyiwa mahojiano
alisema ameficha mabomu mengine huko kondoa na jana alikuwa akipelekwa
kuonyesha ndipo alipotumia trikizake ambazo amefundishwa za ugaidi kwa kupiga
judo na kutaka kuwakimbia askari ndipo akapigwa risasi mbili"alisema Sabas
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kuwafichua waovu
ili kuwaza kuteketeza matukio ya uhalifu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni