Wakati
michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara ikizidi kushika kasi,timu ya Ndanda FC ya
mjini Mtwara imemfukuza kocha wa timu hiyo Dennis Kitambi pamoja na kocha wa
Magoli kipa Mohamed Mwarami.
Akizungumza na Kituo cha
redio cha East Africa, Seleman Kachele amesema wamefikia hatua hiyo baada ya
uongozi kukaa kikao cha dharura na kujadili mambo mbalimbali yaliyopelekea timu
hiyo kufungwa katika mechi zake za Ligi Kuu hivyo wakaamua kuchukua uamuzi huo.
Kachele amesema, timu hiyo
itakuwa chini ya mkurugenzi wa Ufundi Mahibu Kanu mpaka pale watakapopata kocha
wa kuchukua mikoba ya Kitambi na Mwarami.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni