Jamii ya wapenzi wa jinsia moja
pamoja na watu waliobadili jinsia zao nchini Kenya inataka serikali
kulazimishwa kulipatia usajili shirika walilozindua kutetea masilahi yao.
Wanasema ikiwa serikali itakosa kufanya
hivyo itakuwa ni ukiukwaji wa haki zao.
Katika kesi yao waliyofikisha
mahakamani, kundi hilo linasema haki zao zimelindwa na katiba ambayo inajali
utu , usawa na haki pomoja na kuwaruhusu watu kushirikiana.
Kundi hilo linasema kuwa ni ukiukwaji
wa katiba ya Kenya kwa serikali kukataa kusajili shirika hilo la wapenzi wa
jinsia moja.
Kulingana na stakabadhi
zilizowasilishwa mahakamani, shirika hilo, linasema kwa watu wa jinsia moja na
wale wanaotaka kubadili jinsia yao wanapaswa kusajiliwa ili waweze kutetea
maslahi yao.
Hata hivyo serikali inasisitiza kuwa
shirika hilo linapaswa kutimiza matakwa ya usajili wa mashirika yasiyo ya
kiserikali ambayo yanasema kuwa kila anayetaka kusajiliwa lazima apate idhini
ya mkurugenzi wa sekta ya mashirika yasiyo ya kiserikali.
CREDIT: BBC/SWAHILI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni