Makabidhiano ya bati yaliyofanyika nje zinapojengwa ofisi za chama cha mpira Mkoa wa Njombe ( Njolefa) kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa shirika la Tanwat Rajeev Singh, Edymund Munubi afisa tawala wa Tanwat, Katibu wa Chama cha Mpira Mkoa wa Njombe Steven Njowoka na wa Mwisho ni Afisa Utamaduni na michezo Mkoa wa Njombe Steven Sanga. Picha na James Festo.
Waandishi wa habari kazini
Mkurugenzi wa kampuni ya Tanwat, Rajeev Singh akisalimiana Macho.
Ni mfano wa mbao 77 ambazo zilitolewa na Mmiliki wa shule ya Hagafilo Bw Edward Mwalongo wa kwanza kushoto.
Diwani wa kata ya Uwemba Bw Edward Mwalongo (kutoka kushoto) wa pili ni Katibu wa chama Mkoa Bw Njowoka , Raymond Ngondola mkurugenzi wa shirika la Jr fire familigation na mwisho ni Afisa utamaduni Mkoa Bw Sanga.
Na Mwandishi Wetu, Njombe.
CHAMA chama cha mpira Mkoa wa Njombe kimepokea mchango wa bati, saruji na mbao wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni moja kutoka kwa wadau wa michezo zitakazazosaidia kuendelea kujenga ofisi zao ngazi za mkoa. Akiongea katika makabidhiano katibu wa chama hicho Steven Njowoka alisema kuwa wamepokea michango kutoka kwa wadau ambapo hapo juzi walifanikiwa kupokea bati 53, Mifuko ya saruji kumi na mbao 77 vyote vyenye thamani ya shilingi milioni 1,295,000/= na kufanya jumla ya michango kutoka kwa wadau wa michezo kufikia shilingi milioni 1,891,000/=. Njowoka aliendelea kuwaomba wadau mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Njombe kuendelea kuchangia mchango utakaokifanya chama hicho mkoa wa Njombe kukamiliisha ujenzi wa ofisi zenye vyumba saba vilivyofikia hatua ya kupauliwa kwani hivi sasa wanafanya kazi katika jengo ambalo wamepangishwa.
"sisi kama chama cha mpira bado tunahitaji kusaidiwa ...lengo letu ni kuwa hosteri yenye uwezo wa kulaza wachezaji na unapotaka kuchangia usiangalie sura ya Njowoka angalia Njorefa inafa inahitaji nini kutoka kwako"alisema Katibu wa Njorefa. Katibu huyo aliwataja wadau wakubwa waliotoa michango hiyo kuwa ni pamoja na Mkurugenzi wa shirika la Tanwat Rajeev Singh ambaye alitoa Bati zenye thamani ya shilingi laki nane, Diwani wa kata ya Uwemba Bw. Edward Mwalongo ambaye alichangia mbao zenye thamani ya shilingi 355000/= na Mkurugenzi wa kampuni ya Jr fire familigaion Bw Raymond Ngondola alitoa mifuko kumi ya saruji yenye thamani ya shilingi 140,000/=.
Naye Afisa Utamaduni na michezo Mkoa wa Njombe Steven Sanga alitumia fursa hiyo kuwakumbusha viongozi wa timu mbalimbali kuhakikisha wanaweka mipango madhubuti itakayoifanya michezo kusonga mbele ikiwa pamoja na kufuata taratibu na kubainisha kuwa viwanja vingi vya michezo Mkoani hapa vinamilikiwa na taasisi za elimu hali ambayo inawalazimu kuanza kufanya marekebisho ili kuvitumia katika michezo.
Nao baadhi ya wadau hao, Rajeev Singh na Raymond Ngongola aliwasihi wazazi kuachana na itikadi ya kudhani michezo ni uhuni badala yake kuanza kufikiria kuwa michezo huchangamsha akili ya mwanafunzi na kuahidi kuendelea kukichangia chama hicho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni