Bw Aloyce Ntukamazina Meneja Masoko kutoka katika Mfuko wa GEPF akifafanua jambo kuhusu mafao yatolewayo na Mfuko wa GEPF katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, Arusha.Mwanachama mpya akipata maelekezo ya namna ya kujiunga na Mfuko wa GEPF kutoka kwa Afisa wa GEPF Bi Jane Rutashobya katika maonesho ya wakulima ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro, ArushaAfisa Masoko Clement Oningo akitoa maelezo kuhusu shughuli za Mfuko wa Mafao ya Kustaafu wa GEPF kwa wakazi wa jiji la Arusha waliofika katika banda la GEPF.
Muonekano wa banda la GEPF katika viwanja vya nane nane jijini Arusha.Meneja Masoko Aloyce Ntukamazina , Alitoa wito kwa wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya nane nane ili kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huo. “Nawasihi wananchi wajitokeze kwa wingi katika maonyesho haya na kuja kutembelea katika banda letu na kuweza kupata elimu na faida za kujiunga na mfuko huu”alisema Ntukamazina.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni